tiko
tiko
MSANII wa
Bongo Fleva, Ommy Dimpoz na mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan,
mapema leo walifanya tukio la kipekee baada ya kutinga katika shule ya
Mbezi High School, waliosoma na kuwashitukiza walimu na wanafunzi kwa
pamoja kabla hawajaingia kwenye vipindi vya masomo.
Wakizungumza katika ishu hiyo, Ommy
Dmpoz na Idris walisema walikutana na kukaa pamoja na kujadiliana juu
ya kwenda shuleni hapo kuwapa moyo na shukurani kwa ujumla walimu na
wanafunzi wa shule hiyo ambayo walisoma.
“Tumekaa na tukapanga hili wazo ili
tuweze kuwashukuru kwa yote mnayotutendea, hususani kufuatia ushindi
wangu wa Big Brother, ambao naamini kabisa kwa vyovyote mchango wenu
ulikuwa mkubwa kwangu. Mwenzangu Ommy Dimpoz alitangulia kumaliza shule
kabla yangu, ila mmekuwa mkimsapoti kwa kila anachokifanya kwenye
muziki wake,” alisema Idris.
tiko
tiko
Post a Comment