tiko
tiko
Hakika wikiendi iliyopita ilikuwa ni
shangwe tupu, lakini kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia leseni ya
Chadema, Zitto Zuber Kabwe ilikuwa ya machungu pale alipojikuta akimwaga
chozi ukumbini.
Mpango mzima ulioshuhudiwa na paparazi
wetu ulijiri kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo
Bendi ya Malaika, chini ya Christian Bella ilikuwa ikishusha burudani ya
kufa mtu.
Wakati Mbunge wa Jimbo la Sikonge
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Said Nkumba alitesa kwenye jukwaa la
Msondo Ngoma pale TTC Chang’ombe, Temeke, Zitto alifunika vibaya Mango
Garden, Kinondoni, kwani alikuwa zaidi ya shabiki, pedeshee na mwimbaji.
Katika muda ambao watoto wa mjini husema
ni usiku mnene, Zitto ambaye yupo katika mgogoro na chama chake,
alipanda jukwaani wakati prezidaa wa Malaika Band, Christian Bella
‘Obama’ akiimba wimbo wake mpya wa ‘Nani Kama Mama’ ambapo mheshimiwa
huyo alichotwa na hisia za kibao hicho hadi kujikuta akimwaga machozi
kwa kumbukumbu ya msiba wa mama yake mzazi uliotokea mwaka jana (Shida
Salum, alifariki Juni 1, 2014 jijini Dar es Salaam).
Mh. Zitto Kabwe akiteta jambo na wanamuziki wa Bendi ya Malaika.
“Lilikuwa ni tukio la kushangaza kwa
mheshimiwa, maana alipanda stejini kisha akajiunga na waimbaji,
akachukua gitaa na kuanza kucharaza kana kwamba alifanya nao mazoezi,”
alisema shabiki mmoja ukumbini hapo,
Hata hivyo, baadaye mwanasiasa huyo
kijana kipenzi cha wengi, aliimarika na kuendelea kuuimba wimbo huo huku
akiserebuka kwa kwenda mbele.
Baada ya kuona hivyo, mashabiki walimiminika jukwaani kupiga naye picha kwa muda wa takriban dakika 20, ambapo mbunge huyo alithibitisha kuwa ni mtu wa watu kwani shughuli zote zilisimama kwa muda ukumbini humo.
Baada ya kuona hivyo, mashabiki walimiminika jukwaani kupiga naye picha kwa muda wa takriban dakika 20, ambapo mbunge huyo alithibitisha kuwa ni mtu wa watu kwani shughuli zote zilisimama kwa muda ukumbini humo.
Katika hali hiyo, mapedeshee, ambao
hung’ara katika kumbi kwa kutunza waimbaji na wanenguaji, walizimwa
ngebe zao kwani Zitto alifunika kwa kutoa ‘mshiko’ wa kufa mtu.
Ilifahamika kwamba, Bella peke yake alipokea zaidi ya noti 50 za elfu kumi-kumi za Kitanzania kutoka kwa Zitto huku nyingine zikiwa ni dola za Kimarekani.
Ilifahamika kwamba, Bella peke yake alipokea zaidi ya noti 50 za elfu kumi-kumi za Kitanzania kutoka kwa Zitto huku nyingine zikiwa ni dola za Kimarekani.
Wakipiga picha ya pamoja.
Hata hivyo, katika hali nyingine, baadhi
ya watu walihoji usalama wa Zitto kuwa ni sawa na sifuri katika kipindi
hiki ambacho bado sakata la kashfa ya uchotwaji wa mabilioni kwenye
Akaunti ya Escrow ya Tegeta linaendelea kushika kasi na vigogo
kufikishwa mahakamani.
Watu hao walisema kwa namna Zitto
alivyoingia ukumbini hapo na kujichanganya na mashabiki, ni rahisi kwa
mtu mwenye nia mbaya kuweza kumdhuru, hasa watu wa Escrow ambao wana
mapesa yanayoweza kuwashawishi kumfanya lolote.
“Watu wanatetemeshwa na hili skendo, leo
wakimuona Zitto hapa kajiachia namna hii, watakumbuka jinsi
alivyosimama kidete bungeni kutaka waliohusika wawajibishwe na fedha
zirudishwe, unadhani nani hajui utamu wa fedha,” alisikika shabiki mmoja
akisema.
Zitto alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili kupata maoni yake juu ya usalama wake, lakini iliita bila kupokelewa.
tiko
tiko
Post a Comment