Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MASTAA: WATOTO KWANZA, NDOA SIYO ISHU

tiko tiko
WAKATI mastaa kadhaa wa kike wa filamu Tanzania wakionekana umri wao kuwatupa mkono, lakini wakiwa hawana ndoa wala watoto, baadhi yao wamefunguka kuwa wanahitaji zaidi kupata uzao kuliko kuishi maisha ya kuolewa.
Staa wa filamu wa filamuBongo, Anti Lulu akipozi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, walisema suala la ndoa ni majaaliwa na si jambo unaloweza kupanga, kwa vile mwenye uwezo wa kufanya hayo yote ni Mungu, kama ilivyo katika kuamua kuzaa au la.
Coletha Raymond ‘Koletha’, alisema katika maisha ya Kitanzania, wanaume ndiyo wenye uwezo wa kuamua. wataoa lini na ikawa kwa sababu wao ndiyo wanaotongoza, lakini mwanamke hawezi kusema.
“Kuolewa natamani sana lakini bado sijapata mwanaume sahihi, naendelea kumuomba Mungu anipe, nawaomba na wengine wanisaidie kuomba, kuhusu kuzaa niko tayari hata kama sijaolewa,” alisema.
Staa wa filamu wa filamuBongo, Baby Madaha.
Kauli kama hiyo ilitolewa pia na msanii wa filamu Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ aliyesema yupo tayari kuzaa hata kabla ya ndoa kwa sababu kuitwa mama kwake ni muhimu kuliko ndoa.
Lakini katika hatua ya kushangaza, Baby Madaha ambaye pia anafanya muziki, alisema hana anachotamani kati ya ndoa wala mtoto, isipokuwa kitu muhimu kwake kwa sasa ni pesa.
Staa wa filamu wa filamuBongo,Salma Jabu ‘Nisha’.
“Katika maisha yangu sina mpango wa kuolewa  wala kuzaa, ninachotafuta zaidi ni pesa na umaarufu, dunia nzima initambue, sijali cha umri wala nini, hayo ndiyo maamuzi ya maisha yangu.”
“Mimi siwezi kujua nitaolewa lini kwa sababu Mungu ndiye anajua ubavu wangu uko wapi na anakuja kwangu lini, pia siwezi kuwa na uhakika kama niliyenaye  ndiyo ubavu wangu.
“Naweza nikasema naolewa mwaka huu kumbe nikaja kuolewa  miaka miwili mbele. Suala la kuzaa kiukweli hakuna kitu natamani sasa hivi kama mtoto, hili sizungumzii sana, litakuwa ni sapraizi kwa mashabiki zangu,” alisema Tamrina Poshi.
Staa wa filamu wa filamuBongo, Coletha Raymond ‘Koletha’ akipozi.
Kwa upande wake, Salma Jabu ‘Nisha’ alisema ndoa ni heshima kwa mwanamke, lakini anachoamini jambo jema hupangwa na Mungu.
“Mungu anatengeneza tutakayerandana na kupendana kiukweli na kuja kudumu kama wazee   wetu walivyokuwa, akimleta hata leo nitaolewa,” alisema.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top