tiko
tiko
Mbunge wa Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema
Mbunge
wa Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema amesema atamtoa kwa mabavu
bungeni Waziri wa nishati na madini,Profesa Sospetre Muhongo katika
kikao kijacho cha Bunge endapo atakuwa hajaondolewa kwenye nafasi hiyo.
Mkakati
huo wa Lema umeungwa mkono na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema),
Joshua Nassari ambaye pia amepanga kumtoa bungeni kwa nguvu, Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge.
“Keshokutwa
nakwenda bungeni kufanya kazi moja tu, nikimkuta Muhongo bungeni ndipo
nitafukuzwa ubunge moja kwa moja,” alisema Lema huku akishangiliwa
wananchi na kuongeza; “Nikimkuta Muhongo bungeni na Chenge bado ni
viongozi mimi nitakwenda kumshika Muhongo nimtoe bungeni kwa sababu
Katiba inaruhusu kila raia kukemea uovu.”
Profesa
Muhongo na Chenge ni miongoni mwa viongozi ambao Bunge liliazimia
wawajibishwe na mamlaka zao kutokana na kashfa ya uchotwaji mamilioni ya
fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Hata
hivyo, wakati Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Taifa, Desemba 22 mwaka
jana kupitia wazee wa Dar es Salaam, alitangaza kumweka kiporo Profesa
Muhongo kwa siku mbili au tatu, ahadi ambayo haijatekelezwa.
Tayari
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema anayehusishwa
na sakata hilo alishatangaza kujiuzulu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akifutwa kazi.
Kauli ya Lema
Akihutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika Viwanja vya Relini mjini
Moshi, Lema alisema Januari 27 mwaka huu ataingia bungeni akiwa na lengo
moja tu la kumtoa kwa mabavu, Profesa Muhongo.
“Eti Tibaijuka kapewa tu bilioni moja kaondoka, waziri mwenye dhamana hajavuliwa nyadhifa. Rais Kikwete vipi?” alihoji.
Lema
alidai kwamba sakata hilo, katibu binafsi wa Rais ambaye hata hivyo
hakumtaja kwa jina, ndiye aliyeandika barua kuruhusu fedha za escrow
zitoke lakini hadi sasa yuko salama na hajawajibishwa.
Pia,
alihoji sababu za Jaji Werema kutofikishwa mahakamani wakati ndiye
aliyefanya makosa katika kutoa ushauri uliozaa sakata la escrow badala
yake watu wadogo ndiyo wanashtakiwa.
“Leo
tunaona watu wanapelekwa mahakamani, Rais Kikwete nikuulize swali,
ulisema siyo fedha za Serikali ni za watu binafsi mbona mnashika watu
mnawapeleka mahakamani?” alihoji Lema.
Alisema
Sh306 bilioni za escrow zingeweza kujenga nyumba 15,000 za walimu,
kununua mashine 300 za CT -Scan na kujenga barabara ya lami yenye urefu
wa kilomita 600 lakini zimeliwa na wachache.
Kauli ya Nassari
Akihutubia,
Nassari alisema yupo bega kwa bega na Lema katika kumtoa kwa nguvu
bungeni Profesa Muhongo, huku akisema Bunge lijalo litawaka moto.
“Lema umesema hapa ukimkuta Muhongo bungeni uko tayari kuvuliwa ubunge na mimi si mdogo wako? Tuko pamoja,” alisema na kuongeza:
“Nitamwambia
Lema kaba kule na wewe Sugu (Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini)
kaba kule halafu mimi narukia pale kwenye Siwa, tunaondoa Siwa
tutamfuata Muhongo alipo,” alisema.
Nassari
aliwataka wananchi wa Moshi kufuatilia kikao hicho cha Bunge na akisema
haiwezekani maazimio ya Bunge yasitekelezwe kwa ukamilifu wake na kwa
wakati.
tiko
tiko
Post a Comment