tiko
tiko
UKATILI, Mtoto mchanga ambaye anasadikika kuwa wa siku saba, amekutwa akiwa ameuawa na mwili wake kuwekwa kwenye mfuko wa rambo kisha kutupwa pembeni mwa jalala. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Mtaa wa Kaloleni katika Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya .
Wakizungumza na gazeti hili mashuhuda
ambao hawakupenda majina yao kuandikwa gazetini walisema kuwa walimkuta
mtoto huyo akiwa amenyongwa kisha kuwekwa kwenye karatasi ya naironi
(rambo) .
Waliongeza kuwa mtoto huyo alitambulika
baada ya watoto wadogo wakiwa katika michezo yao katika maeneo yao
kuuona mfuko huo wa rambo na kuufungua ndipo wakatoa taarifa wa wazazi
wao,” alisema mmoja wa wazazi wa eneo hilo.
“Hiki kitendo ni kibaya sana na
aliyefanya unyama huu anastahili adhabu kali. Huwezi kulea mimba miezi
tisa kisha unamza mtoto na kumnyonga shingo hadi kufa, ni ukatili
uliokithiri, tena mtoto huyu ni kama wa siku saba, hii ni kwa sababu
kitovu chake kilionesha dalili za kupona,” aliongeza.
Hata hivyo, aliyefanya kitendo hicho cha kikatili hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
“Tunaomba wenye kujua aliyefanya haya
atuletee jina ili tumkamate,” alisema ofisa huyo bila kutaja jina lake
kwa kuwa siyo msemaji wa polisi. Msemaji wa jeshi hilo mkoani Mbeya ni
SACP Ahmed Msangi (pichani).
tiko
tiko
Post a Comment