tiko
tiko
Rapper
Kalapina ambaye anatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuusaka
ubunge wa jimbo la Kinondoni, amesema kuwa akipata fursa hiyo hatosita
kusambaza kichapo kwa wabunge wenzie pindi wanapokuwa na malumbano ndani
ya mjengo.
Akiongea
kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Kalapina amedai kuwa
atatembeza ‘nakozi’ kwakuwa anatambua hakuna sheria inayoweza kumbana
kutokana na kufanya tukio kama hilo.
“Vitasa
kidogo, wewe ile hela imepigwa Tegeta huko na Tegeta hakuna mtu
kachukua hata shilingi, vitasa vingetembea,” alisema. “Nafikiri ulimuona
mheshimiwa Sugu, si unatetea watu na mbunge ndani ya bunge huwezi sijui
kupelekwa mahakamani, masula yanamalizwa kibunge,” aliongeza.
“Kwahiyo
ngumi bungeni zipo, mabunge yote duniani, sema bunge letu halijapata
wale watu ambao wanaweza kupigana vita na mtu mwenyewe ni Kalapina
mgombea wa Kinondoni ninayeingia mjengoni, Jamanii eeh jipangeni, nakuja
huko.”
tiko
tiko
Post a Comment