Mwanamke mmoja nchini Misri ameamua kukatiza na gauni la arusi mitaani kupinga masimango anayokutana nayo kwa kuchelewa kuolewa. Samah Hamdimwenye miaka 27 alifikia
uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kashfa kutoka kwa watu wanaomzunguka
ikiwemo familia yake hasa mama yake mzazi ambao wamekua wakimsema
kutokana na kutokua na mume mpaka sasa. Hamdi
ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili alisema ameamua kutembea
hivyo mitaani na kamwe hawezi kuacha dhamira yake hiyo ikiwa kama
ishara ya kupinga mila na desturi inayowakandamiza wanawake wasioolewa.
Samah Hamdi akiwa anatafakari jambo huku akiwa amevaa gauni lake la harusi katika moja ya mitaa jijini Cairo
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook
ukijiunga na mimi
Post a Comment