tiko
tiko
Msanii wa filamu anayeonekana kuwa moto,
Ester Kiama amefunguka kuwa, wanaodhani ameingia kwenye fani ya
uigizaji ili kutafuta wanaume wamebugi kwa kuwa yeye siyo mburula na
hajui hata anaanzaanzaje kufanya hivyo.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni,
Ester alisema wakati alipokuwa nje ya fani alikuwa hapati usumbufu
lakini sasa ameamua kuonyesha kipaji chake anaonekana kama ameingia
kujiuza kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wasiojitambua.
“Mimi bwana siyo mburula, nimeingia
kwenye filamu ili kuonesha kipaji changu na wala si kuja kuuza sura wala
kujiuza, wanaojiuza ni haohao, hivi mimi naanzaanzaje?” alisema Ester
ambaye amefanya kweli kwenye filamu ya Ngoma Ngumu inayotarajiwa
kuingia mtaani wakati wowote.
tiko
tiko
Post a Comment