tiko
tiko
UKISTAAJABU ya
Musa utayaona ya Firahuni! Binti aliyefahamika kwa jina moja la Afsa
(14), anayesoma darasa la 7, ametiwa nguvuni na jeshi la polisi akidaiwa
kuwafanyia ukatili na kuwadhalilisha watoto wawili wa kiume (majina
kapuni) wa mama yake mkubwa kwa kuwakang’ata nyeti zao akiwalazimisha
kufanya nao mapenzi.
Tukio hilo la kushangaza ambalo lilijaza
umati wa watu , lilitokea wiki iliyopita katika mtaa wa Nyerere, Kata
ya Mafisa, mkoani hapa.
Kamanda wa OFM, Mkoa wa Morogoro akiwa kazini, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi wa mtaa huo wakimuomba afike fasta.
Bila kuchelewa kamanda alitia timu na kukutana na akina mama wawili ambao walishusha ‘vesi’ za tukio hilo:

“Sisi ni wakazi wa mtaa huu wa Nyerere
ambao tunaishi na Mama Mese mwenye watoto wawili wa kiume, anaishi pia
na mtoto wa mdogo wake (Afsa) aliyempa jukumu la kuwalea wanaye.
“Cha kushangaza Afsa amekuwa akiwafanyia ukaliti wa kutisha watoto hao. Leo amewatoboa macho na njiti ya viberiti kuwapiga mateke na kuwasukumiza ukutani, mbaya zaidi aliwang’ata nyeti zao alipokuwa akiwalazimisha kuduu nao.

“Kama majirani tumemuuliza mama Mese
inakuwaje wanaye wanateswa kila siku na yeye hachukui hatua yoyote,
akasema hataki kwenda polisi wala kwa mwenyekiti wa mtaa anaogopa mtoto
wa mdogo wake atafungwa sasa sisi tumeamua kukuita uje kushudia tukio
hili bichi,” walisema kina mama hao walioomba hifadhi ya majina.
Mwanahabari wetu alifika kwenye nyumba
hiyo na kumkuta mama Mese akiwa na watoto wake hao wakiwa na makovu
mwili mzima, alipoulizwa undani wa tukio hilo na kwa nini hatoi taarifa
katika vyombo vya usalama? Alifunguka:
“Mimi ni mfanyakazi pia mwanafunzi,
nasoma chuo hivyo wanangu hulelewa na Afsa ambaye ni mtoto wa mdogo
wangu. Kweli wanangu wamepigwa na kufanyiwa ukatili na huyu mtoto wa
mdogo wangu lakini suala hili sitaki lifike popote, nimepanga kumrudisha
kwao Moshi,” alisema Mama Mese.
Katika hali ya kushanga, paparazi wetu alipotaka kumhojia Afsa, mama huyo alikataa jambo lililowakera majirani na kuibua vurugu.
Katika hali ya kushanga, paparazi wetu alipotaka kumhojia Afsa, mama huyo alikataa jambo lililowakera majirani na kuibua vurugu.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, jirani mmoja
aliwatonya polisi ambao walifika ndani ya muda mfupi na kufanikiwa
kumkamata Afsa kumpeleka kituoni kwa ajili ya hatua za kisheria huku
mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Yusuf Juma akishuhudia tukio hilo na
kulilaani.
tiko
tiko
Post a Comment