tiko
tiko
Imeripotiwa kuwa watu watatu wamefariki dunia mkoani hapa katika matukio tofauti yakiwemo mawili ya mauaji ya kinyama.
Miongoni
mwa matukio ya mauaji hayo ni pamoja na la mkazi wa kijiji cha Mkutano
wilayani Momba, Hamis Simwawa (25) aliyekutwa shambani akiwa ameuawa kwa
kukatwa shoka shingoni na kisha kunyofolewa viungo vya mwili ikiwemo
ulimi, meno ya chini na jicho la kushoto.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki alisema mwili wa Hamis
ulikutwa Januari 26 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji
cha Mkutano kilichopo katika kata ya Nzoka wilayani Momba.
Kaimu
Kamanda Masaki alisema kabla ya mauaji kijana huyo aliitwa kwenda
kusaidia shughuli za shamba na alipofika shambani ndipo walimuua kwa
kumkata na shoka shingoni kabla ya kumnyofoa ulimi, meno ya chini na
jicho la kushoto na kupeleka viungo hivyo kusikojulikana.
Alisema
tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina ambapo Kawawa Sinkala
(31) na Emmanuel Sinkala (15) wakazi wa kijiji cha Mkutano wanashikiliwa
na polisi kuhusiana na mauaji hayo.
Katika
tukio la pili, Kaimu Kamanda Masaki alisema Mwinzala Sekele mwenye umri
wa kati ya miaka 40 na 45 mkazi wa kitongoji cha Chang’ombe kilichopo
kijijini Mshewe wilayani Mbeya aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za
mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Alisema
mwili wa marehemu ulikutwa Januari saa kumi na moja alfajiri ukiwa
umetelekezwa kijijini mshewe kata ya Bonde la Usongwe wilayani Mbeya.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda Masaki inadaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo ni
kulipiza kisasi kufuatia Sekele kutuhumiwa kuhusika na mauaji
yaliyotokea awali Januari 24 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri ambapo
mkazi wa kijiji cha Mshewe Sekela Kaini alikutwa ameuawa na mwili wake
kutupwa kwenye shamba la mahindi kijijini hapo.
Katika
tukio lingine mkazi wa Ilomba jijini Mbeya Joshua Mwaisanila (35)
alifariki dunia baada ya kugongwa na lori lenye namba T 189 BLKs Semi
Trailler lililokuwa na tela lenye namba T 193 BLK lililokuwa
likiendeshwa na Ahazi Cheyo (24) mkazi wa Iyunga jijini Mbeya.
Kaimu
Kamanda Masaki alisema ajali hiyo ilitokea Januari 26 mwaka huu saa
tatu asubuhi maeneo ya Forest barabara kuu ya Mbeya/ Tunduma na dereva
wa lori hilo anashikiliwa na polisi wakati chanzo cha ajali
kinachunguzwa.
tiko
tiko
Post a Comment