tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
BIFU lililodumu kwa muda mrefu kati ya Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga
Pepeta, Asha Baraka na Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki leo
limemalizika rasmi katika ofisi za Global Publishers Ltd zilizopo
Mwenge, Bamaga jijini Dar.
Juhudi za kuwapatanisha wakongwe hao katika muziki wa dansi zimefanywa
na baadhi ya viongozi wa Global Publishers ambap wanakiri kuwa halikuwa
jambo rahisi kuwapatanisha viongozi hao.
Wakongwe hao katika muziki wa dansi wameamua kumaliza tofauti zao na
kuwa kitu kimoja huku wakiahidi kushirikiana katika muziki na mambo
mengine.
Mbali na mengi yaliyoongea pia wamekubaliana kufanya onyesho la pamoja
huko mbeleni kuwadhihirishia mashabiki kuwa kwa sasa hawana bifu lolote
na wamekuwa kama ilivyokuwa awali.
Mtandao huu unawapongeza na kuwatakia kila la kheri viongozi hao kwa
uamuzi sahii waliouchukua ili kuzidi kusukuma gurudumu la muziki wa
dansi.
(PICHA NA GPL)
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment