tiko
tiko
KICHANGA kinachokadiriwa
kuwa na umri wa miezi nane, wiki iliyopita kiliiokoa familia yake
kuteketea kwa moto, baada ya kuamka usiku na kulilia kunyonya, kitendo
kilichomshtua mama yake aliyebaini nyumba yao ilikuwa ikiungua, huko
Kibamba Lungwe jijini Dar es Salaam.
Akisimulia tukio hilo, mama wa kichanga
hicho, Asha Mohamed, alisema alishtuka baada ya mtoto kuanza kulia
akitaka kunyonya, alipoamka ndipo akaona mwanga mkali juu ya paa, hali
iliyomlazimu kuamka na kwenda kumgongea Abuu ili kutafuta njia ya
kutoka,” alisema mama huyo akiongeza kuwa sebuleni, moto ulikuwa
umetapakaa.
Kijana Abuu Masoud (15), baada ya
kuamshwa, alionyesha ujasiri na upendo mkubwa kwa kujitoa mhanga
kuwasaidia wadogo zake watatu waliokuwa wamelala katika moja ya vyumba
vya nyumba hiyo.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, alifanikiwa kumtoa mtoto mmoja.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, alifanikiwa kumtoa mtoto mmoja.
“Nilipofungua mlango wa sebuleni nikaona
moto na moshi mwingi sana, roho iliniuma sana kwani chumba cha pili
kulikuwa na wadogo zangu watatu wamelala, nikaamua kuvaa ujasiri na
kujitosa katika chumba kile na kufanikiwa kutoka na mtoto mmoja,
wakabaki wawili,
baada ya kurudi ndani nikapata wazo la
kuzima Mean switch, nilipoenda kuishika ikaniangukia kichwani kwani
ilikuwa imeshaungua, ndiyo nikaungua na kushindwa kuwatoa waliobakia,
ingawa baadaye kuna msamaria mwema mmoja alijitokeza na kuja kubomoa
mlango na kuwatoa wengine,” alisema kijana huyo.
Mama wa mtoto mchanga alifanikiwa kutoka pasipo kudhurika.
Aidha baba mwenye nyumba hiyo, Khalfani Maketemo, ambaye wakati nyumba yake inaungua yeye na mkewe walikuwa hospitali alikokuwa amelazwa, anadai chanzo cha moto huo ni shoti iliyoanzia kwenye bati na anaamini ni kutokana na kuunganishwa vibaya kwa waya unaopitisha umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba.

Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya
majirani walisema; “Uunganishwaji wa umeme ni wa kubabaisha, waya
unagusana na bati jambo ambalo ni hatari kama waya utachubuka na mvua
kunyesha’’.Familia hiyo kwa sasa haina sehemu ya kujisitiri nyumba nzima
imeteketea.
tiko
tiko
Post a Comment