tiko
tiko
MWANAUME mwenye
imani ya Kirasta ambaye jina lake halikuweza kunaswa mara moja,
mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akinyolewa rasta zake bila ridhaa
yake kufuatia kudakwa akidaiwa kutaka kuiba kwenye duka moja.
Nywele za rasi zikiwa hatarini kuchezea wembe wa 'NACET' kama si 'GILLETE'
Tukio hilo lililokusanya watu kibao, lilijiri maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam chini ya jengo jipya la Wanyama.
Kwa mujibu wa mashuhuda, rastaman huyo alipofika kwenye duka hilo alijifanya kutaka kununua bidhaa mbalimbali kwa kuulizia bei zake lakini mtu mmoja dukani humo aliyekuwa akimlia ‘rada’ kwa mbali aligundua kuwa jamaa hakuwa mteja bali mkwapuzi.

“Ilikuwa kufumba na kufumbua, jamaa
akiwa katika hatua ya mwisho kukwapua, akaitiwa mwizi na kudakwa
hapohapo huku kipondo kikianza kumshukia mwilini.
“Alitolewa nje ya duka, watu wakajaa wakisema apigwe mawe hadi kufa, wengine apelekwe Kituo cha Polisi Msimbazi, lakini kuna mtu akasema hakuna haja ya adhabu zote hizo, kwa kuwa ana nywele za kirasta dawa ni kumnyoa.

“Huwezi amini, jamaa alijitetea kuwa
yeye si mwizi lakini wembe wa Gillete ulinunuliwa, watu wakaanza kumnyoa
nywele kwa kukata yale mabutu ya kirasta,” alisema shuhuda mmoja.
Mwisho wa tukio hilo, rasta huyo aliachiwa kwa vile iliaminika kuwa, adhabu aliyopewa ilimtosheleza kama si kumtia adabu.
Mwisho wa tukio hilo, rasta huyo aliachiwa kwa vile iliaminika kuwa, adhabu aliyopewa ilimtosheleza kama si kumtia adabu.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa
wamiliki wa maduka Kariakoo alisema changamoto kubwa ya biashara maeneo
hayo ni wizi wa mara kwa mara.
“Hapa tunaibiwa kila siku. Kuna siku tunawakamata siku nyingine wanafanikiwa bila kukamatwa. Wanatupa hasara sana hawa watu.
“Hapa tunaibiwa kila siku. Kuna siku tunawakamata siku nyingine wanafanikiwa bila kukamatwa. Wanatupa hasara sana hawa watu.
“Mfano akikuibia suruali ya shilingi
elfu thelathini maana yake amekata faida ya suruali kama tano. Sasa hapo
huo umeme wa Tanesco tutalipaje na vibarua tutalipaje?” alihoji
mfanyabiashara huyo bila kutaja jina lake.
tiko
tiko
Post a Comment