tiko
tiko
Mwenyekiti wa ACT,Kadawi Limbu
Chama
cha ACT-Tanzania kimewasimamisha viongozi wa chama hicho ambao ni
Mwenyekiti wa muda Kadawi Limbu na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Leopold
Mahona na kikimvua madaraka Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana, Grayson
Nyakarungu.
Hatua
hiyo imejitokeza baada ya maazimio ya Halmashauri Kuu iliyokutana
kujadili agenda za nidhamu ya mwenyekiti, kupokea na kupitisha mwongozo
na kanuni za uchaguzi pamoja ushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Katibu
mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba alisema jana kuwa maazimio ya
mkutano huo yaliwachagua Shaaban Mambo kuwa mwenyekiti wa muda, Mohamed
Masaga, Naibu katibu mkuu na Hassan Abdalah Omary kuwa mwenyekiti mpya
wa vijana.
“Mkutano
wa jana (juzi) ulikuwa na wajumbe 65, lakini kura 57 zilipendekeza
Limbu na Mahona wasimamishwe katika nafasi zao kwa muda,” alisema
Mwigamba na kuongeza kuwa: “Kwa mujibu wa katiba ya chama, Kifungu cha
27(f) kinasema halmashauri ina mamlaka ya kuwasimamisha kwa kipindi cha
miezi sita, baada ya hapo watakuwa na haki ya kugombea tena nafasi zao
pindi uchaguzi utakapoitishwa.”
Alipoulizwa kuhusu uamuzi huo kama wameshawapatia na kuwajulisha wahusika, Mwigamba alisema tayari taratibu zote zilishafanyika.
“Kwanza
tuliwapa nakala ya mashtaka pia tukawaita kwenye mkutano ili kuwapatia
nafasi ya kujitetea. Limbu alikataa kujieleza,” alisema Mwigamba.
Hata
hivyo, chama hicho kwa siku za hivi karibuni kimekuwa katika mvutano
kati ya Limbu na viongozi wenzake, hasa katibu mkuu, akidaiwa kuhujumiwa
na vyama vikubwa vya siasa.
Akizungumzia
uamuzi huo, Limbu alisema siyo sahihi kwani mkutano huo hauna mamlaka
ya kumwondoa kwenye nafasi yake bali ni kamati kuu tu ndiyo ina uwezo
huo.
“Sheria
ya vyama vya siasa ndiyo inatoa mamlaka. Wajumbe waliokaa hatuna
uhakika kama wamefikia akidi ya 65 kama tulivyoelezwa,” alisema Limbu.
tiko
tiko
Post a Comment