tiko
tiko
Jeshi la polisi
mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kibara wilayani Bunda
mkoani Mara Jonathani Daniel (33) kwa tuhuma za kupatikana na noti
bandia 75, za shilingi elfu kumi kila moja zenye thamani ya shilingi
750,000, pamoja na vifaa vya kutengenezea pesa hizo bandia.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa Polisi mkoani
Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Desemba 27
mwaka huu,majira ya saa 2:00 usiku katika eneo la kituo cha basi kwenye
kijiji na kata ya Kakola tafara ya Msalala wilayani Kahama.

Amesema
mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa jeshi hilo wakati wakiwa katika
doria ya kawaida kwenye kituo hicho cha mabasi akiwa na noti hizo bandia
na kuwa kati yake noti 3 zina namba BL, 0315207, noti (32) BB 0315203, noti (21) BE 0315206 , na noti (19) zikiwa na namba BC 0315209.
Kamanda
Kamugisha ameongeza kuwa licha ya kumkamata mtuhumiwa na noti hizo
bandia, pia amekamatwa akiwa na bando ya karatasi , Sindano pamoja na
chupa ya konyagi iliyokuwa na unga mweupe, vifaa ambavyo vinasadikiwa
kutengenezea noti hizo.
Aidha kamanda
Kamugisha ameongeza kuwa Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa
mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazo mkabili mara baada ya
upelelezi wa jeshi hilo kukamilika.
tiko
tiko
Post a Comment