tiko
tiko
Mtu
mmoja Timotheo kweka (30) mkazi wa kiwanja cha ndege manispaa ya
Morogoro amekutwa chumbani kwake amefariki dunia siku nne ziizopita na
jeshi la polisi limelazimika kuvunja mlango na kutoa mwili huo .
Akizungumza
na ITV mmiliki wa nyumba alikokuwa amepanga Leonard Benedicti amesema
kwa mara ya mwisho marehemu alionekana nje siku ya jumamosi hadi leo
walipohisi harufu nzito chumbani kwake ndipo walitoa tarifa kwa jeshi la
polisi na kumkuta ndani amefariki na kichwa kikiwa kimebanwa kwenye
stuli.
Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa
marehemu wamesema hawanawasiwasi na kifo cha ndugu yao kwani alikuwa
mlevi wa pombe kwa muda mrefu ambapo wamesema siku ya jumamosi walikuwa
na sherehe ya ukoo lakini marehemu hakuweza kufika ingawa hawakujua kama
amefariki.
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro
limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa
wa morogoro.
tiko
tiko
Post a Comment