tiko
tiko
Bongofleva
ilipofikia sasa hivi ni kwenye kubadilisha maisha ya Watanzania wengi
wenye juhudi na ambao angalau wanalipwa na muziki wao ambapo ni mara
nyingi tumekua tukizipata stori hapa millardayo.com na kwenye AyoTV jinsi mastaa wanavyotoa ushuhuda wao.Hii stori ya leo ya rapper Young D inagusa hisia sana hasa ukizingatia udogo wa msanii huyu mwenye umri wa miaka 21 tu lakini aliweka BIG NO kwenye mahitaji yake mengine yaliyokua yanamsubiri alafu akaamua kukwangua kila kitu kwenye account yake ili kufuta machozi ya familia hasahasa ya mama yake mzazi.
Hii nyumba aliiweka kwenye page yake ya instagram @Youngdaresalama na vyombo vya habari vikachukua hizo picha na kuripoti kwamba kanunua nyumba ila ukweli ndio huu.
Yafuatayo ni mambo nane aliyoyasema Young D kuhusu hii stori…
- Ni nyumba ambayo walikua wakiishi zamani na Marehemu baba yao aliefariki mwaka 2008 akiwa ni mzee Mstaafu.
-
Baba yao aliugua sana kabla ya kufariki ambapo wakati wa kuugua
kwake, kwa sababu familia haikua na uwezo ilibidi wachukue mkopo
uliofikia milioni nane ili pesa hizo ziwasaidie kwenye matibabu.
-
Baada ya mzee kufariki familia ilishindwa kulipa deni hivyo ikabidi
benki itangaze kuiuza nyumba hii ambayo familia ilikua imeshakata tamaa
kwamba hawatoweza kuikomboa tena.
- Anasema huu uamuzi wake ulirudisha furaha ya familia kwa kiasi kikubwa sana….. yani walikua wamepewa siku 14 kuikomboa lakini Young D alitumia siku 4 tu kumaliza kulipa hizo pesa.
- D Anasema pesa zote hizo alizokua nazo ni kutokana na muziki peke yake, yani bongofleva anayoifanya ndio ilimlipa kutokana na show za Tour ya Pepsi mwaka juzi pamoja na showz mbalimbali alizofanya.
Kama unapenda stori kama hizi zisikupite, jiunge kwenye familia ya tabasamu na daniel
tiko
tiko
Post a Comment