tiko
tiko
WAKATI Rais
Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za
Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati
mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.
Katika Mtandao wa Twitter, binti huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Kagem Tibaijuka, alimtetea mama yake
akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti yake zilikuwa ni safi na halali
na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya kuwasaidia kielimu watoto wa kike.
“My mum did nothing wrong except wanting
to help young girls get an education. A school built with my late
father. Accepted a donation,” (Mama yangu hakufanya kosa lolote
isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana kupata elimu. Shule ilijengwa na
marehemu baba yangu. Mchango ukakubaliwa)yalikuwa ni moja ya maneno
yake katika mtandao huo wa Twitter.
Aidha, aliwashambulia wanawake
walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete alipotangaza kumuwajibisha
mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa kushangilia anguko la mwanamke
mwenzao na kwamba hata wao iko siku yatawakuta ya kuwakuta.
Lakini katika mitandao mingine ya
kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum inayotembelewa na watanzania
wengi, walimshambulia binti huyo kwa kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha
na kwamba mama yake alistahili kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni
pamoja na kushtakiwa.
Wachangiaji walioonekana kuchukizwa na
utetezi wa binti huyo kwa mama yake, walisema licha ya Profesa Tibaijuka
kuondolewa, pia watu wote waliotajwa, wakiwemo Waziri Sospeter Muhongo
na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi nao walistahili kuondolewa katika nafasi
zao.
Gazeti hili lilimtafuta mama Tibaijuka
kupitia simu zake mbili za mkononi, ili kuzungumzia maoni yake baada ya
kukutwa na ajali hiyo ya kisiasa pamoja na kumuuliza kama Kagem ni
bintiye, lakini moja iliyopatikana, iliita kwa muda mrefu bila
kupokelewa. Hata hivyo baadaye simu hiyo ilipopigwa, ilionekana
imezimwa.
Aidha Kagem mwenyewe, ambaye ofisi zake
zinadaiwa kuwa eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, naye hakupokea
simu yake ya mkononi aliyopigiwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa
maneno, hakujibu.
Jumatatu iliyopita, Rais Kikwete
alizungumzia suala hilo la fedha zilizodaiwa na Bunge kuwa ni za umma,
kuchukuliwa isivyo halali katika akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya
Tanzania. Wakati Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema alijiuzulu
mwenyewe na mama Tibaijuka kuwajibishwa, viongozi wengine waliodaiwa
kuhusika na fedha hizo wanaendelea kuchunguzwa na hatua stahiki dhidi
yao zitachukuliwa.
tiko
tiko
Post a Comment