Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

WATU 38 WAFARIKI DUNIA KWA MVUA YA MAWE KAHAMA, SHINYANGA

tiko tiko
Muonekano wa nyumba baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na  upepo  mkali kunyesha katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani shinyanga.
Baadhi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mvua hiyo.
Mbuzi wakiwa wamepoteza maisha baada ya kupigwa na mvua ya mawe.
WATU 38 wamefariki Dunia huku wengine zaidi ya 60 wakijeruhiwa vibaya baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana  upepo  mkali kunyesha katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka Wilayani Kahama Mkoani shinyanga.

Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa march tatu majira ya saa tatu za usiku na kusababisha maafa hayo ambayo hayajawahi kutoka katika Mkoa wa Shinyanga.

Kamugisha katika maafa hayo watu 35 walifariki papo hapo huku majeruhi zaidi ya 60 wakikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya kupatiwa matibabu na jitihada zaidi za uokozi zikiendelea katika kijiji hicho

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Joseph Ngowi akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa amepokea majeruhi zaidi ya 60 na kati yao watatu wamefari wakati wakiendelea na matibabu katika Hospitali hiyo.

“Hatuna idadi kamili ya watu waliojeruhiwa au waliokufa na tumetuma madaktari wetu kwenda katika kijiji hicho kwa ajili ya huduma ya kwanza pamoja na kufanya uchunguzi ili kubaini idadi kamili ya waliofariki Dunia”, Alisema Joseph Ngowi.

Dr, Ngowi alisema kuwa kutokana na umbali uliopo kutoka katika eneo la tukio hadi katika Hospitali ya Wilaya wamelazimika kutuma jopo la madaktari kwenda kwenye eneo la tukio ili kubaini waliofariki na kuhidhinishwa kwa maziko ili kupunguza gharama kwa wananchi waliofiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya inategemea kukaa mchana huu kwa ajili ya kutathimini takwimu za uharibifu wa mali pamoja na idadi ya nyumba zilizokumbwa na maafa hayo.

Alisema kuwa Jeshi la zima moto kwa kushirikiana na Wananchi wanaendelea na shughuli za uokoaji na huenda idadi ya waliokufa  pamoja na majeruhi ikaongezeka katika tukio hilo.

Hata hivyo Majeruhi waliolazwa katika Hspitali ya Wilaya ya Kahama wakizungumzia  kuhusu tukio hilo walisema kuwa Mvua hiyo ilionyesha kwa upepo mkali ulioambatana na mawe makubwa  hali iliyosababisha uliosababisha nyumba kuezuliwa pamoja na kung’olewa kwa miti.

“Tulikuwa tumelala majira ya saa tatu usiku ghafla tulisikia upepo mkali ukiambatana na mvua kubwa ya mawe na maji  mengi kuingia ndani na ghafla nyumba yangu ilianguka na kupoteza wajukuu wangu wanne,” alisema Paulina Malongo mmoja wa majeruhi waliolazwa katika Hospitali hiyo.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top