tiko
tiko
Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.
Katika
tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa amelewa sana na kwamba
walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh Mziwanda,ghafla sehemu aliyokuwa
amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa chupa ambayo ilikuwa ikimlenga
msanii huyo bahati nzuri aliikwepa ikampiga jamaa mmoja lakini
haikumjeruhi.
Baada
ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie juu Shilole na kumuuliza
kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole alianzisha ugomvi na
kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua kukaa pembeni peke
yake na kuanza kulia.
‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh
sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana
kiukweli alileta fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu
walikuwa kwenye sherehe hiyo.
Baada ya hapo msanii Quick Racka
alimfuata Shilole na kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo
aliamka na kumrushia chupa ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye
aliikwepa ikapasuka chini.
Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu Shilole kumsomea
mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo alikuwa amelala.
Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh Mziwanda kwa
kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi karibuni alimpiga
vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za viwanja vya Leaders na
baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia vyombo vya habari na
kuahidi kutompiga tena.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment