tiko
tiko
Mwalimu
wa shule ya Sekondari Kibasila, Gaudensia Albert aliyekuwa akihifadhi
kinyesi ndani kwake kwa miaka miwili amepelekwa Hospitali ya Muhimbili
baada ya daktari wa Hospitali ya Temeke kubaini ana matatizo ya akili.
Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Kyando amesema baada ya kugundulika kwa
tukio hilo walimpeleka Hospitali ya Temeke kwa kuangalia afya yake
ambapo daktari akasema ana tatizo la akili, wakamuhamishia Muhimbili.
Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari walimpatia dawa ambazo anatumia
mpaka sasa pamoja na ushauri. “Sisi bado tunamhitaji kutokana na tatizo
la uhaba wa walimu wa sayansi ulioko nchini”—alisema Mwalimu Kyando na
kuongeza kuwa mbali na tatizo la kukutwa na kinyesi bado mwalimu huyo
alikuwa anafundisha vizuri.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment