tiko
tiko
JESHI
 la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha kuhusika kwa Idara 
 Usalama wa Taifa katika mipango ya kutaka kumuua Katibu mkuu wa chama 
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dokta Wilbroad Slaa.
  Kauli
 ya jeshi la polisi kanda hiyo ni kama  inamjibu Mjumbe wa kamati kuu ya
 CHADEMA (CC), Mabere Marando ambaye katika taarifa yake kwa vyombo vya 
Habari alimtuhumu Naibu mkuu wa idara ya Usalama mkoa wa Kinondoni 
Elisifa Ngowi kuandaa mipango miovu kwa dokta Slaa akishirikiana na 
Mlinzi wa Katibu huyo bwana Khalid Kagenzi pamoja na Makumu mwenyekiti 
wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara,Philip Mangula.
  Akikanusha
 taarifa hizo leo Jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Polisi Kanda maalum 
ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati na mkutano na vyombo vya Habari 
amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi wakina ikiwemo kuchukua taarifa 
upande wa chama cha Chadema na Mlinzi wa Dokta Slaa na kubaini hakuna 
ukweli idara ya Usalama wa Taifa kuhusika.
  “Tumefanya
 uchunguzi wa  kina ikiwemo kuwahoji watu wote wanaotuhumiwa .Tumebaini 
kwa dhati kabisa hakuna mtu yeyote wa usalama wa Taifa aliyehusika 
katika mipango ya kumdhuru Dokta Slaa", Amesema Kamishna Kova.
  Kamishna
 Kova ameongeza kuwa kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi wa suala 
hilo na uchunguzi ukikamilika watafawakisha wahusika  wote  mahakamani 
bila  kumwogopa mtu yeyote.
  Katika
 hatua nyingine, Jeshi hilo linawashikiria watu wawili wanaojiita  
viongozi wa watu waliopata mafunzo ya mgambo kwa kosa la kuratibu na 
kuongoza vikao vya uchochezi vya mgambo dhidi ya serikali.
  Kamishna
 Kova amewataja watuhumiwa kwa majina kuwa ni  Mathias lubega miaka 
43,mkazi wa Bunju ambaye amekamatwa maeneo ya Mission Pup huko Mbagala 
Mkoa wa Polisi Temeke.
  Wa pili ni Mohamed  Ally miaka 38 naye pia ni mkazi wa Mbagala .
  Mbali
 na kuwakamata watuhumiwa hao,kamishna Kova alithibitisha kuwa jeshi 
hilo katika msako wake mkali limefanikiwa kukamata  noti bandia za dolla
 za kimarekani zipatazo 426 ambapo noti 36 ni za dolla 100 na noti 390 
ni za dolla 50.
  Kamishna
 kova pia aliwataja kwa majina watuhumiwa ambao pesa hizo zilikutwa kwao
 kuwa ni Ramadhani Mhambo miaka 34,mkazi wa Mwanayamala jijini Dr 
,Eliazr Jackob Nkurarumi na Juma Mohamed mrundi miaka 25 ambaye ni 
mlinzi  wa Colombia Hoteli.
Mbali
 na watuhumiwa hao, Kamishna Kova aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni 
Rajabu Nassor miaka 30 ambaye ni fundi simu,Mkazi wa mwananyamala kwa 
sindano ambapo wote wakuwa kwenye makazi yao walikutwa na fedha hizo 
bandia.
tiko
tiko


 
 
 
 
 
 
Post a Comment