tiko
tiko
Mpaka sasa ndani ya Marekani ni majimbo matatu ambayo wametoa ‘YES’
kuruhusu matumizi ya marijuana au bangi, Washington DC, Alaska na
Colorado, lakini wataalamu wanasema kuna majimbo mengine ambayo yako
njiani kuhalalisha matumizi hayo.
Barney Warf
ni professor wa Chuo Kikuu cha Kansas, anasema ni ngumu kutabiri kuhusu
jimbo lipi na lipi litahalalisha matumizi ya dawa hizo za kulevya,
lakini majimbo haya matano aliyoyataja hapa kuna dalili zote bangi ikawa
halali kwao, kutokana na kwamba kwa sasa bangi inatumika kama dawa
nyingine za matibabu, hiyo kwake ni hatua ya kwanza kwenye kuelekea
kuhalalisha matumizi kwa mtu yoyote.
Majimbo hayo ni California, Nevada, Vermont, Illinois na New York ambako Prof. Warf anasema muda si mrefu tutarajie kupitishwa kwa Sheria ya matumizi ya bangi kama kilevi cha kawaida ambacho kimehalalishwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment