tiko
tiko
MBUNGE
wa Mbinga Magharibi (CCM), John Komba, amefariki dunia kutokana na
kuzongwa na mzigo wa madeni, likiwamo mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Taarifa
zinasema, benki hiyo ilitoa kiasi cha sh. 12 bilioni kwa mwanasiasa
huyo mwaka 2009, lakini hadi mauti yanamkuta, alikuwa hajaweza kulipa
deni hilo.
Habari
zinasema, wakati Komba akihaha kuokoa nyumba yake kutokana na tanganzo
la benki ya CRDB kwenye vyombo vya habari; huku akiwa tayari ameonekana
kukata tamaa; ghafla Jumamosi jioni alipatwa na shinikizo la damu na
kufariki dunia.
mamilioni
hayo ya shilingi yalitolewa na CRD Benki kwa mbunge huyo kwa ajili
ajili ya kuendeleza shule zake mbili alizokuwa akizimiliki – shule ya
Sekondari ya Bakili Muluzi na Shule ya Msingi ya Coletha – zilizoko
jijini Dar es Salaam.
Hadi
anafariki dunia, Komba alikuwa amebakiza kiasi cha zaidi ya sh. 78.5
milioni. Deni la Benki linatokana na mkopo pamoja na riba ya asilimia 17
katika kipindi cha miaka mitano ya uhai wa mkopo.
Komba amefariki dunia Jumamosi iliyopita, miezi mitatu baada ya Benki ya CRDB kuuza shule zake.
Mbali
na kuuza shule, benki iliuza vifaa mbalimbali, likiwamo eneo la ukubwa
wa mita za mraba zaidi ya 34,000 lililotumika kutoa mkopo wa sh. 900
milioni mwaka 2009.
Shule za Komba pamoja na vifaa vyake, vimenunuliwa na mfanyabiashara mmoja mmoja.
Gazeti
hili limeelezwa kuwa Komba alijaribu, bila mafanikio, kushawishi
serikali kununua shule yake; na kwamba alitinga hadi ikulu na makao
makuu ya CCM kuomba msaada ili shule na nyumba yake visiuzwe.
Hata
hivyo, taarifa zinasema, Komba hakufanikiwa kupata msaada wa kuzuia
shule kuuzwa. Hadi anafariki dunia benki ilikuwa inajiandaa kuuza nyumba
yake.
“Yule
bwana alifika hadi ikulu kuomba msaada ili nyumba yake isiuzwe. Alitaka
serikali imsaidie kununua shule yake; au kuomba benki izuie kwa muda
uuzaji kwa kuwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilikuwa
limekubali kununua eneo hilo kwa bei ya soko,” ameeleza mtoa taarifa.
Baada
ya shule kuuzwa na deni kushindwa kumalizika, mtoa taarifa anasema,
Komba alirudi tena ikulu na CCM kuomba msaada wa kukwamua nyumba yake.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, alijaribu kunusuru shule ya Komba kupigwa mnada kwa
kuiandikia benki ya CRDB kumpa mwanasiasa huyo muda zaidi wa nyongeza
ili kulipa deni lake.
Hata hivyo, pamoja na maombi ya Pinda kupewa nafasi, bado Komba alishindwa kulipa deni hilo.
Komba
aliyekuwa anajulikana kwa jina maarufu la “Mzee wa kutoa mitaji kwa
vimwana,” alizikwa juzi Jumanne, katika jimbo lake la uchaguzi la Mbinga
Magharibi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment