tiko
tiko
Binti wa miaka (14) aliyefahamika kwa 
jina la Latifa amejikuta akisutwa kwa utapeli baada ya kunaswa na OFM 
akijifanya ni mtoto asiye na wazazi wala ndugu wa kumsaidia.Binti huyo 
aliwasimulia waandishi wetu kuwa baba yake alimtelekeza kwa majirani 
huko Dodoma maeneo ya Kibaigwa kwa kile alichodai kuwa baba yake alikuwa
 na madeni yaliyosababisha mali zake kupigwa mnada na yeye kusakwa ndiyo
 maana alikimbia.
Latifa alisimulia kuwa kwa kuwa hakuwa 
na ndugu yeyote aliyekuwa akimfahamu alilazimika kuishi maisha magumu ya
 kuhamahama akiwa peke yake ambapo alidai alikimbilia kwa ndugu wa baba 
zake mkoani Lindi ambapo huko alikutana na kasumba ya ukeketaji na 
kukimbilia jijini Dar.
Akiwa Dar Latifa aliwasimulia waandishi 
wetu kuwa alikuwa akifanyishwa kazi nyingi kama hausigeli ndani ya 
nyumba moja maeneo ya Tegeta ambapo pamoja na hayo alikuwa akinyanyaswa 
sana.
Alizidi kudai kuwa aliamua kukimbilia 
Kijitonyama akiwa kama mzururaji ambapo alikutana na madada wanaojiuza 
ambao alidai kuwa walimchukua na kuishi naye mpaka alipokutana na 
waandishi wetu ambao aliwaomba msaada kwa madai hakuwa na chakula wala 
mahali pakulala .
AANZA KUSHTUKIWA
Hata hivyo, baada ya kupelekwa kwa mfadhili aliyeahidi kumpa malazi binti huyo, alimshangaza mwenyeji wake kwa kupigiwa simu mara kwa mara na watu ambao hakuwaweka wazi. Alipopekuliwa kwenye simu ndipo namba za watu waliogundulika kuwa ni ndugu zake walionekana na walipopigiwa walikiri kumfahamu Latifa kama ndugu yao na kuanika siri kwa nyakati tofauti kuwa kweli Latifa hana mama lakini tabia za utapeli zimemfanya afukuzwe kwa kila ndugu anayeishi naye.

“Yaani huyo mtoto hakuna mtu anayetaka 
kuishi naye mimi mwenyewe ameshaniliza na simtaki aje kwangu, nyie cha 
msingi mtoeni hapo nyumbani kwenu yasije yakawakuta,” alisema kaka yake 
aliyejitambulisha kwa jina la Saidi kauli iliyotiliwa mkazo na mama yake
 mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Mwazani.
Hata hivyo, waandishi wetu waligundua 
kuwa msichana huyo kwa nyakati tofauti alienda nyumbani kwa wasanii wa 
filamu, Wema Sepetu, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael kwa nia ya 
kutaka wamasaidie lakini kashitukiwa na kutimuliwa.
“Nilienda kwa Wema nikagonga akatokea 
msichana akaniambia Wema hayupo nikawa narudia mara nyingi lakini 
mwishoni akanifokea. “Nikaenda kwa Lulu lakini mama yake alinifukuza na 
kwa Wolper niliambiwa alipokuwa akiishi alishahama,” alisema msichana 
huyo aliyedai yote aliyofanya ni kutokana na ugumu wa maisha hivyo 
asitiriwe.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko

Post a Comment