tiko
tiko
MSANII mkongwe
katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu
atakayekamata kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana
matusi ya nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe,
Sajuki.
Akizungumza na gazeti hili, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi ya
mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo
zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha
Sajuki.
“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki
kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai
kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui
nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume
wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na
mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment