tiko
tiko
Wachezaji kadhaa wa klabu ya Manchester United wanafanyiwa uchunguzi baada ya kuhusishwa na tukio la kutengenezwa kwa mkanda wa ngono lililofanyika ndani ya ukumbi wa starehe wa usiku .
Mwanamke mmoja ambaye hajatajwa amerekodiwa akiwa anafanya vitendo vinavyoshahibiana na ngono huku akiwa na mmoja kati ya wachezaji wa Manchester United ambaye si raia wa England kwenye choo cha klabu ya usiku huku moja kati ya wachezaji wenzie akiwa anarekodi tukio hilo kutokea juu ya mlango .
Mwanamke aliyehusika kwenye tukio hilo alihojiwa na gazeti moja la kila siku huko England ambako alielezea jinsi alivyofedheheshwa na tukio hilo ambapo alisema kuwa tangu wakati huo amekuwa akilia na hakutaka kueleza zaidi juu ya kilichotokea .
Mwanamke huyo ana hofu ya kuwa wachezaji wengine wa kikosi cha United wanamfahamu na wataonyeshana video inayoonyesha kitendo hicho kitendo ambacho kitamshushia heshima .
Klabu ya United haijatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili na hadi sasa hakuna mchezaji ambaye ametajwa kuhusishwa na tukio hilo .
tiko
tiko
Post a Comment