tiko
tiko
Kuna neno la Kiswahili watu wengi huwa
wanalitumia, “usimdharau mtu usiyemjua”, kutokana na shughuli za kila
siku tunakutana wengi sana tusiofahamiana nao barabarani.
Nchi za wenzetu zile treni za umeme
zinazoenda kasi ni usafiri muhimu sana, watu wengi wanazitumia kama
ambavyo sisi tunatumia daladala hivi, sasa jamaa mmoja ambaye ni kama
aliianza siku vibaya aliingia kwenye treni London, mtu mmoja akawa
amesimama mbele yake kama kamzuia hivi, jamaa hakupenda hiyo, akamsukuma
halafu akamtukana.. safari yao ikaendelea.
Mchana jamaa huyo alikuwa na Interview
ya kazi, ishu ikawa kwenye jopo la wanaomhoji mmoja wao alikuwa yule
jamaa ambaye alimktukana asubuhi kwenye treni, Matt Buckland ambaye ndie aliyetukanwa anasema moja ya swali ambalo alimuuliza ilikuwa hili; “nilimuuliza kama alisafiri poa kwenye treni asubuhi ya leo.. Tulicheka kwa pamoja halafu nikamuomba radhi”
Buckland aliandika kwenye ukurasa wake Twitter kuhusu ishu hiyo, hii ni moja ya Tweets zilizopata Retweets nyingi pamoja na favourites pia.
Jamaa ambaye alikutwa na noma hiyo jina lake halikufahamika, Buckland amesema jamaa huyo alikosa nafasi hiyo ya kazi sio kwa kuwa alimtukana ila kwa sababu alikosa vigezo vilivyotakiwa.
Karma - the guy who pushed past me on the tube and then suggested I go F myself just arrived for his interview...with me...
— Matt Buckland (@ElSatanico) February 16, 2015
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook
ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment