tiko
tiko
Uteuzi wa Makonda ni fimbo kwa mafisadi.Asibezwe anaweza.
Anaitwa Paul Makonda.Ni Katibu wa Hamasa
na Chipukizi wa Uvccm.Kijana mdogo mwenye ujasiri wa kipekee asiyeogopa
kejeli,dharau na fitna za mafisadi.Kwasasa ndio Mkuu wa wilaya ya
Kinondoni.
Jamii ya wenye akili inashangaa
wanaobeza uteuzi wa rais kwa Paul Makonda.Inawashangaa wanaomponda Paul
Makonda.Haijajulikana hadi sasa nia na sababu zenye mashiko zinazotumika
kumchafua Paul Makonda.Vijana wanaombeza ndio haohao wanaoomba kila
siku kuwa vijana wapewe nafasi katika vyombo vya maamuzi.
Kumponda Paul Makonda ni kudharau uteuzi
wa rais wa nchi.Rais anatambua umuhimu wa vijana kupewa nafasi.Anatoa
fursa kwa vijana.Hili ni jambo la kupongezwa sana.Ni hatua kubwa na
nzuri kwa ukuwaji wa demokrasia nchini.
Paul Makonda kaaminiwa.Mnalalamika kila
siku kuwa kina January na Kigwangallah au Mwigulu wasibezwe tena wao
wanaomba nafasi kubwa ya urais.Lakini Paul Makonda kupewa Udc mnaona
kama kapendelewa na hawezi.Sisi tunaamini Paul Makonda anaweza na wilaya
aliyopewa aiongoze ataimudu,aungwe mkono kwa asilimia mia moja.
Kelele za mafisadi zisiondoe imani kwa
vijana wasiowaunga mkono.Paul Makonda anapinga ufisadi.Ni
jasiri.Mpiganaji wa kweli dhidi ya maovu.Kambi za urais
zisiwapotoshe.Wanaomsema hovyo wamepoteza dira ya kisiasa na
kimaisha.Wana political stress isiyotibika inayotokana na kukosa maadili
ya uongozi na kisiasa.
Abarikiwe Paul Makonda.Abarikiwe aliyemteua.Ibarikiwe Ccm.Ibarikiwe Tanzania.Ibarikiwe Kinondoni.Viva Paul Makonda "Jembe".
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment