Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

TAMASHA LA PASAKA LASAMBAA MIKOA 17

tiko tiko
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Alex Msama. 
Na Mwandishi Wetu
IDADI ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka, sasa imefikia 17 kwa mujibu wa waandaaji.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ilisema kuwa idadi hiyo ni kubwa na haijawahi kutokea tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao. Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali kwa wadau wetu wa huko.
 “Lakini si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa,  Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.
Alisema kamati yake inatarajiwa kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika mwaka huu.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu waanzishe tamasha hilo.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII

tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top