Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MOTO WATEKETEZA MADUKA YA WAFANYA BIASHARA JIJINI TANGA

tiko tiko

 
Maduka ya wafanyabiashara mbali mbali yaliyopo mtaa wa india jijini Tanga yameteketea kwa moto kwa kile kinachodaiwa kuwa imetokana na hitilafu ya umeme.

Moto huo uliokuwa ukifukuta ndani katika maeneo hayo ya biashara ulisababisha baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo kutaka kulishambulia gari la zima moto la halmshauri ya jiji la Tanga kufuatia kufika katika eneo la tukio lakini wakati linaaza zoezi hilo ghafla likaishiwa na maji katika kipindi cha dk 3 na kuamsha hasira kwa mamia ya wananchi.
Hata hivyo akielezea hatua hiyo kamanda wa opesheni wa kikosi cha zima moto mkoani tanga Bwana Kumenya Bakari amekemea vikali jazba za wananchi za kushambulia mara kwa mara gari la zima moto la halmashauri ya jiji  la tanga na kufafanua kuwa wanapofika katika eneo la tukio jambo la kwanza wanaanza kwanaza kuokoa maisha ya watu,mali ndio kisha baadae kuzima moto katika eneo husika.

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII


tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top