tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YANGU!..

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida familia tatu zenye watu 16 katika kijiji cha Mikese mkoani Morogoro wanalazimika kulala nje kwa siku saba mfululizo baada ya nyumba wanazoishi kuwaka moto mara kwa mara na kuunguza samani za ndani na vyakula.
Inaelezwa kuwa chanzo cha moto huo hakifamahamiki na hivyo kusababisha hofu kwa familia hizo kutaka kuyakimbia makazi yao.
Mwandishi wa habari hizi amefika katika
familia hizo na kuona vitu mbalimbali vilivyoungua moto vikiwemo
vyakula nguo madaftari ya wanafunzi huku wakinamama na watoto pamoja
na wazee wakiwa nje.
Wananchi hao wamesema katika hali
isiyokuwa ya kawaidia moto huo huwaka zaidi ya mara tisa kwa siku na
wanajaribu kuuzima lakini chanzo cha moto huo hakieleweki ingawa
nyumba hizo hazina umeme wala nishati ya aina yoyote inayosabaisha
moto.
Wananchi hao wamefananisha tukio hilo
kama la miujiza na kuomba watu wenye imani mbambali kufika na kufanya
maombi katika nyumba hizo kwani wanateseka kwa kushindwa kulala ndani.
Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha
Lukole Ramadhani Shaban amekiri kuwepo kwa matukio ya moto kuwaka
katika nyumba hizo kwa siku saba mfululizo.
Amesema siyo tukio la kawaida na
jitihada wanazozifanya kama serikali ya kijiji wameanza kuwatafuta
wachungaji na mashekhe ili kusaidia kufanya maombi katika nyumba
hizo kwani familia hizo zinaishi katika mazingira magumu ya kulala nje
kwa muda mrefu.
Via>>Itv
Via>>Itv
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment