tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YANGU!..
Msafara
wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla
kuelekea kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha
Mvomero.
Mbunge
wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa
amepakiwa kwenye pikipiki (Bodaboda) wakati akielekea kwenye kitongoji
cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.



Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla jana
alifanya ziara katika Jimbo lake hilo kwa kutumia usafiri wa pikipiki
kufika kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero
ambacho kwa historia hakijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote tangu uhuru.
Mbunge huyo ambaye amesifika na kuweka rekodi ya kutembelea vijiji vyote
130 vya Jimbo lake hilo,aliona umuhimu kuwafikia wananchi na wana CCM
wa Ifumbo kwa njia ya pikipiki ili ajionee changamoto na kuchukua hatua
stahiki ili kukabiliana nazo.
Makalla alifika kwenye kitongoji hicho cha Ifumba na kulakiwa kwa
shangwe na wananchi wa kijiji hicho ambao walifurika kwa wingi kumpokea,
na amehaidi kutuma watalaam wa halmashauri wafike na kuiona barabara na
kuingiza katika mipango.
Aidha alikagua ujenzi wa shule ya msingi Ifumbo na kuchangia mifuko 100
ya saruji kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo,pia amesaidia
timu ya Ifumbo Star jezi na mpira na kuwahamasisha kujiandikisha kwenye
daftari la wapigakura pindi litakapoanza.
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment