Waziri
wa maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyarandu amefunguka kuhusiana na
taarifa zilizoenea kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu
za Kibongo,Aunty Ezekiel na kwamba ujauzito alionao msanii huyo ni wa
kwake.Mh.Nyalandu
amekanusha habari hizo kupitia kupindi cha leo tena cha Clouds Fm
wakati alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho Husna Abdul
ambapo pia alikuwa ameambatana na mkewe Faraja Kota.Aidha
alisema kuwa habari hizo zilitolewa na gazeti moja la hapa nchini kuwa
waziri huyo atumia mamilioni ya pesa za umma kuponda raha na msanii
huyo,wakati huo alikuwa nchini Marekani kikazi kwa mwaliko wa ubalozi wa
nchini humo ambapo wasanii wawili wa hapa nchini Aunty Ezekiel na
Kassim Mganga nao walikuwa wamealikwa. ‘’Kwa
mara ya kwanza nilimuona msanii huyo kwenye mwaliko huo na baada ya
hapo nikaondoka zangu sikuonana naye tena hata namba yake sina hapo
ndipo habari zikaenea kuwa nimetembea naye mara mimba aliyonayo ni yangu
kwa kweli nilishangaa sana,’’alisema Nyalandu. ‘’Naamini taarifa hizo
zilizidi kuzungumzwa zaidi na maadui zangu wa kisiasa baada ya mimi
kutangaza nia ya kugombea urais uchaguzi mkuu ujao,’’alisema Nyalandu. Hata
hivyo Faraja akizungumzia kuhusiana na taarifa hizo alisema kuwa
hazikumshtua hata kidogo kwa maneno kuhusu mumewe amekuwa akiyasikia
sana na ameshayazoea na anampenda sana mumewe.
Post a Comment