tiko
tiko
Yafuatayo ni maswali na majibu kati ya mwandishi wetu Elvan Stambuli na
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape
Nnauye katika mazungumzo yaliyofanyika nyumbani kwake jijijini Dar es
Salaam Jumamosi iliyopita.
Nape
Nnauye akihojiwa na waandishi wa Gazeti la Uwazi pamoja na Global TV.
Kutoka kulia ni Erick Evarist, Elvan Stambuli na Musa Mateja.
UTARATIBU WA KUMPATA MGOMBEA URAIS
Mwandishi: Hivi sasa kuna joto la uchaguzi na hasa kwa nafasi ya mgombea urais wa nchi yetu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mwandishi: Hivi sasa kuna joto la uchaguzi na hasa kwa nafasi ya mgombea urais wa nchi yetu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mtatumia utaratibu gani kumpata mgombea huyo?
Nape: Chama Cha Mapinduzi kina utaratibu wake wa kumpata mgombea urais kwa kutumia katiba, sifa na kanuni zake ( tumezitaja chini) na kwa kuzingatia maadili ya chama. Na kwenye hili ni lazima tutakuwa makini kwa sababu mgombea wa CCM ndiye atakuwa raia wa nchi yetu na pia mwenyekiti wa taifa wa chama chetu.

Huwezi kupata kadi ya chama juzijuzi kisha ugombee urais. Unaweza
kufanya hivyo lakini ni ni lazima ujipime urefu, kama unajiona ni mfupi
kisha ukaweka matofali ili ulingane na mwenzako, sisi tutayatoa na
matokeo yake utayajua.
Mwandishi: Yapo madai kuwa kuna baadhi ya watangaza nia ya kugombea
urais wanamwaga fedha ili kushawishi watu wawachague kuwakilisha chama
chenu, unasemaje kuhusu hilo?
Nape: Kwanza ieleweke CCM haiuzi urais, sasa kama kuna mwanachama
ananunua wapiga kura huko ni kuvunja maadili ya chama na mtu kama huyo
hatutamvumilia. Kama mtu huyo ana fedha nyingi kwa nini asifanye
biashara? Wanachama wanaonunua wanachama wajijuwe kwamba wanapoteza sifa
za kuwa mgombea wa chama chetu.
Nitachowaahidi Watanzania ni kwamba tutawapa mgombea safi, asiye na doa
kwa sababu hatutaki kutumia muda mwingi kumsafisha mtu. Kwanza maji ya
kumsafishia mtu kama huyo hatuna!
ONGEZEKO LA WAPINZANI BUNGENI
Mwandishi: Kila uchaguzi mkuu unapofika tunashuhudia ongezeko la wabunge wa upinzani, huoni kwamba hiyo ni dalili mbaya kwa chama chenu cha CCM?
Mwandishi: Kila uchaguzi mkuu unapofika tunashuhudia ongezeko la wabunge wa upinzani, huoni kwamba hiyo ni dalili mbaya kwa chama chenu cha CCM?
Nape: Kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni siyo dhambi kwa sababu
uimara wao unasaidia CCM. Ongezeko lao linaweza kuwapoteza kwa sababu
wanaweza kuongeza watu ambao ni wajinga, hivyo kudharaulika bungeni.
Kazi ya ubunge ni kuwatumikia wananchi lakini wabunge wengi wa upinzani
hawayajengi majimbo yao na badala yake wanakomaa kudai Serikali ya
Tanganyika. Wapiga kura huwezi kuwaambia hivyo, wao wanataka umeme,
elimu kwa watoto wao, maji na kadhalika. Mbunge mmoja wa upinzani (jina
tunalihifadhi) wakati wenzake wanakazania kupeleka umeme katika vijiji
vya majimboni mwao, yeye anakijenga chama na mpaka sasa kijiji kimoja tu
ndicho alichofanikiwa kuwapelekea umeme.
Mwandishi: Kuna malalamiko mengi huwa yanajitokeza wakati wa kura za
maoni katika chama chenu kwa wagombea ubunge na udiwani kila
unapofanyika uchaguzi mkuu. Mmejipanga vipi kuepukana na malalamiko kwa
wapiga kura wenu mwaka huu?
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye
akisisitiza jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa Gazeti la Uwazi
(hawapo pichani).
Nape: Ni kweli hilo tunalijua. Tulikuwa tukipiga kura za maoni kwenye
kata lakini ikaonekana ngombea mmoja anaweza kuhonga wapiga kura, hivyo
tukajua ni tatizo, tukahamishia kwenye jimbo kwenye mkutano mkuu wa
jimbo nako kukawa na tatizo. Ninachoahidi ni kwamba mwaka huu
tutaboresha kuziba mianya inayolalamikiwa.
Mwandishi: Yapo madai ya rushwa pia kwa wanaowania ubunge na udiwani, hilo unasemaje?
Nape: Niya ya kuboresha mfumo wa kura za maoni ndani ya CCM ni kupunguza kasoro zilizokuwa zikijitokeza huko nyuma. Rushwa kuidhibiti ni kazi kwa sababu siku hizi watu wanaweza kutoa kwa kutumia simu.

UKAWA KUUNGANISHA NGUVU
Mwandishi: Ukawa wanadai kuwa mwaka hu wanaunganisha nguvu katika majimbo ili wawashinde, kwa upande wa CCM hamuoni kuwa hiyo ni hatari kwenu?
Nape: Kwanza elewa kuwa hakuna kiongozi wa upinzani ambaye hajapitia CCM, hivyo tunawajua kuliko wanavyojijua.

Tunajua walivyo dhaifu na sasa hivi kilichowaunganisha ni katiba ya
nchi. Suala hilo litakoma Aprili 30 mwaka huu. Baada ya hapo hakutakuwa
na Ukawa tena na badala yake watapigana makonde. Nasema hivyo kwa sababu
Ukawa ni Chadema, Cuf, NCCR na NLD wote hao wana itikadi au imani
tofauti, hivyo watafarakana tu.
Mfano mzuri ni kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, walifarakana na
kuna baadhi ya mitaa kila chama kilisimamisha kivyake. Angalia Jimbo la
Ubungo (John) Mnyika ni mtu muhimu sana Chadema lakini na Cuf (Julius)
Mtatiro ni mtu muhimu sana katika chama chake, hapo sasa nani atamuachia
mwenzake? Hata kwenye Urais Dk (Wilbroad) Slaa na Profesa (Ibrahimu)
Lipumba vyama vyao vinawaamini, sasa nani atasimamishwa? Ninachosema ni
kuwa Ukawa litakuwa kaburi lao kwani wakishindwa watu wao watakata
tamaa. Ningetishika kama muungano wao ungekuwa unahusu matatizo ya
wananchi. Watagombana tu na sisi tutaingiza mikono kuwagonganisha.
MMOMONYOKO WA MAADILI
Mwandishi: Kuna madai kuwa maadili ndani ya chama chenu yameporomoka sana ukilinganisha na enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, hilo nalo unalizungumziaje?
Nape: Unajua enzi za Mwalimu watu walikuwa wachache na hata wanachama wa CCM walikuwa wachache. Leo tuna wanachama milioni saba, hivyo katika kundi kubwa kama hilo huwezi kukosa watu wenye tabia tofauti, lakini siyo wote hawana maadili.

KAZI NA DAWA: baada ya mahojiano kilifuata kipindi cha kupata viburudisho na kufanya mazungumzo ya kawaida.
Nakiri kuna udhaifu lakini tumeanza kukaza buti kwa kuwataka wanachama
kufuata katiba, sheria na kanuni zetu.Mheshimiwa Katibu Mkuu,
(Abdurahman) Kinana ameshasema wanaokiuka maadili tutabanana nao na
ndiyo maana tukasema hata wale viongozi waliohusika katika sakata la
Akaunti ya Escrow lazima chama kiwashughulikie. Hatutaki wafanye chama
diyo kichaka chao.
Mwandishi: Kuna watu wanadai kwamba hupatani na Mheshimiwa Edward
Lowassa na wengine wanakwenda mbali kwa kudai kuwa huwa unamsema sana,
je ni kweli ni adui yako?
ANA UGOMVI NA LOWASSA?
Nape: (Anatabasamu) Si kweli kwamba mzee Edward ni adui yangu. Ni mtu ninayemheshimu sana na ni rafiki yangu. Nina uwezo wa kwenda nyumbani kwake nikala chakula wakati wowote na hata nikiwa na shida naweza kwenda kumuomba msaada. Ukweli ni kwamba kuna wakati tulikuwa tunatofautiana kimtazamo. Mimi naamini katika kusimamia maadili.

Tusingesimamia maadili, chama kingekufa. Mimi bado kijana, napenda chama
hiki kiendelee kushika dola. Mzee Edward sina ugomvi naye lakini nina
ugomvi na baadhi ya matendo yake. Chama kitakufa kama mtu atakosea na
kuachiwa. Ilinibidi niseme kwa sababu watu wanasahau kuwa mimi ndiye
Katibu wa Itikadi sasa itikadi ni imani ambayo ni tabia.
Siwezi kucheka au kunyamaza nikiona mtu anakwenda kinyume na itikadi za
chama. Niseme tu kwamba mtu yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya
chama ataniona mbaya. Haya maadili yametungwa zamani hata kabla ya mimi
kushika wadhifa huu.
KUJIVUA GAMBA
Mwandishi: Kulikuwa na dhana ndani ya chama chenu ya kujivua gamba, mlifanikishaa malengo yake?
Nape: Kujivua gamba malengo yake hayakuwa kufukuza watu uanachama, la, lengo lilikuwa ni kuongeza uwezo wa chama chetu wa kusikiliza matatizo ya wananchi. Chama chetu kinaongoza serikali. Kama serikali inakosea hatusiti kusema waziri fulani anakosea. Kujivua gamba kulikuwa na maana kubwa kuliko maana iliyotolewa awali.

Kujivua gamba ni pamoja na kuleta vijana katika uongozi. Angalia safu ya
uongozi wa chama chetu sasa. Awali hakuna aliyejua kuwa CCM itabaki
madarakani lakini sasa kila mmoja anajua kuwa chama kitabaki madarakani.
Niseme tu kwamba hatuna uhaba wa wagombea urais na CCM itatoa mgombea
ambaye atakuwa hana doa kama nilivyosema awali.
KUBOMOLEWA JENGO LA CCM LUMUMBA
Mwandishi: Jengo la CCM ambalo Tanu ilizaliwa mmelibomoa, mnataka kujenga kitega uchumi? Na je huoni kuwa mnaharibu kumbukumbu za chama?
Mwandishi: Jengo la CCM ambalo Tanu ilizaliwa mmelibomoa, mnataka kujenga kitega uchumi? Na je huoni kuwa mnaharibu kumbukumbu za chama?
Nape: Kumbukumbu za chama zitalindwa na pale Lumumba hatuharibu
kumbukumbu za Tanu tunachofanya ni kuboresha ofisi. Zamani ofisi ile
ilikuwa ya makuti baadaya ikaezekwa madebe yale yaliyokatwa kama sambusa
na ilikuwa ya miti, haikuwa na umeme wala maji. Tukaboresha tukaweka
mabati kama vigae. Sasa tunataka kuweka ghorofa.
Hatufanyi uwekezaji, pale tunataka kutengeneza ofisi nzuri ya mwenyekiti
wetu wa taifa ambaye ni rais wa nchi. Tukitaka kuweka kitega uchumi
tungeweza kufanya hivyo sehemu nyingine kwa sababu CCM ina viwanja zaidi
ya mia nne sabini hapa Dar es Salaam. Kwa hiyo yanayofanyika pale
Lumumba ni maborosho tu. Hata Dodoma tutajenga ukumbi mkubwa sana wa
kisasa ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu elfu nne kwa mpigo.
KANUNI ZA UCHAGUZI KWA MGOMBEA URAIS WA CCM
Licha ya Nape kutozitaja kanuni za uchaguzi za CCM za mgombea urais, mwandishi wetu alifanikiwa kuzipata.
Licha ya Nape kutozitaja kanuni za uchaguzi za CCM za mgombea urais, mwandishi wetu alifanikiwa kuzipata.
Kanuni hizo za uchaguzi toleo la mwaka 2005 na marekebisho yake ya mwaka
2010 zimeorodhesha sifa 13 za mwanachama anayefaa nafasi ya urais kama
ifuatavyo:
1. Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa kwa kuzingatia uzoefu wake katika uongozi wa shughuli za serikali, umma na taasisi.
1. Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa kwa kuzingatia uzoefu wake katika uongozi wa shughuli za serikali, umma na taasisi.
2. Awe na angalau kiwango cha elimu ya chuo kikuu au elimu inayolingana na hiyo.
3. Awe mwadilifu, asiyetiliwa shaka juu ya matendo yake ya uadilifu mbele ya uso wa jamii ya Watanzania na awe mwenye hekima na busara.
4. Awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza Muungano, umoja, amani na utulivu na mshikamo wa kitaifa.

5. Awe mtu mwepesi wa kuona mbali, asiyeyumbishwa na mwenye uwezo wa
kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala nyeti na muhimu ya taifa kwa
wakati unaofaa.
6. Awe na upeo mkubwa na usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa ili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi na dunia yote kwa ujumla.
6. Awe na upeo mkubwa na usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa ili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi na dunia yote kwa ujumla.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya udikteta au ufashisti, bali awe
anaheshimu na kulinda katiba ya nchi, sheria, utawala bora, kanuni na
taratibu za nchi.
8. Awe mtetezi wa wanyonge, haki za binadamu, mzingatiaji makini wa
maendeleo ya raia wote na asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wa mtu
binafsi.
9. Awe mstari wa mbele kuzifahamu, kuzitetea na kuzitekeleza sera za CCM na Ilani ya CCM ya Uchaguzi.
10. Awe mpenda haki na mtu jasiri katika kupambana na dhuluma na maovu yote nchini.
10. Awe mpenda haki na mtu jasiri katika kupambana na dhuluma na maovu yote nchini.
11. Asiwe mtu ambaye anatumia nafasi yake ya uongozi kujilimbikilia mali.
12. Kwa ujumla awe ni mtu anayekubalika kwa wananchi.
12. Kwa ujumla awe ni mtu anayekubalika kwa wananchi.
13. Awe mtu makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa
viongozi/ watendaji na asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa
majukumu/ wajibu aliokabidhiwa ili kuinua nidhamu ya kazi, tija na
ufanisi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Filed Under:
SIASA
Post a Comment