tiko
tiko
Nianze kwa kumshukuru Maulana kwa
kunijalia kuiona siku hii ya leo nikiwa mzima wa afya. Ni matumaini
yangu kwamba na wewe msomaji wangu uko poa kabisa, karibu jamvini
tubadilishane mawazo na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa
kimapenzi.
Imewahi kukutokea kwamba licha ya kuwahi
kumpenda au kupendana na mtu fulani, imefika hatua mambo yote hayawezi
kuendelea tena, moyo umekinai, hisia zimekufa na jambo pekee unalotaka
litokee ni wewe na mwenzi wako kuachana?
Kwamba huamini kama kuna jambo lolote
linaloweza kuwafanya mkaendelea kukaa pamoja tena, dunia yenu ya mapenzi
imefika mwisho na hakuna tena cha ziada! Hakuna kipindi kigumu kama
hiki, hasa kama mtu unayeachana naye uliwahi kumpenda au yeye aliwahi
kukupenda.
Kuangukia katika penzi la mtu fulani siyo jambo gumu ingawa hakuna jambo gumu kama kuachana na mtu. Wengi huwa wanashindwa kuukubali ukweli, matokeo yake wanasababisha matatizo ambayo yangeweza kuzuilika mapema.

Sishauri watu waachane isipokuwa
nachotaka kujadiliana na wewe msomaji wangu ni namna bora inayoweza
kutumika kumaliza penzi ambalo haliwezi tena kuendelea. Tunashuhudia
kila siku watu wakiachana kwa matatizo makubwa, wakifanyiana ugomvi
mkubwa, kupigana, kutukanana, kutoleana kashfa za kila aina, eti kisa
mapenzi yamefika mwisho.
Unafikiri ni sawa kuachana kwa vurugu
kiasi hicho wakati mliwahi kuishi pamoja kwa amani, upendo na mahaba ya
nguvu? Nini huwa kinasababisha baadhi ya watu wanakuwa na tabia za aina
hii?
HUO SIYO MWISHO WA MAISHA
Inapotokea umefanya kila kitu kulitetea penzi lako lakini imeshindikana, ni busara kuukubali ukweli kwa sababu mwisho wa mapenzi siyo mwisho wa maisha. Huwezi kujua Mungu anakuepusha na nini, kubaliana na hali halisi kwa sababu inatokea na wewe siyo wa kwanza kuachwa au kukataliwa na umpendaye.
Cha msingi ni kujitahidi kutulia, maumivu yapo tena makali lakini ni vyema kujua namna ya kukabiliana na hali hii ngumu bila kusababisha matatizo zaidi. Mlikutana kwa amani, mkapendana lakini penzi lenu halikupangwa kudumu, kubali matokeo na usonge mbele bila kumfanyia mwenzi wako vurugu.

MPE HAKI YAKE
Kingine ambacho kinatajwa kusababisha ugomvi kwa wanandoa au wapenzi walioishi kwa kipindi kirefu wanapoachana, ni mgawanyo wa mali au vitega uchumi vilivyopatikana mkiwa pamoja.
Wanaume ndiyo wanaotajwa zaidi kuwanyanyasa wanawake wanaoachana nao kwa kukataa kabisa kugawana vitu vilivyochumwa pamoja. Hakuna haja ya kukomoana, mpe haki yake ili na yeye huko anakokwenda, akayaanze vizuri maisha yake.

Kubalianeni wenyewe nani achukue kitu
gani, hakuna haja ya kupelekana mahakamani au kuanza kusumbuana kwa vitu
ambavyo mnaweza kuvimaliza kwa kutumia busara. Narudia tena kusema
kuachana ni jambo baya linaloumiza lakini kuna muda huwa unafika,
mnakosa njia nyingine mbadala zaidi ya kuachana.
Kama mlijaliwa kupata watoto, kubalianeni jinsi ya kuendelea kuwalea watoto bila matatizo. Kubaliana na ukweli na maisha yataendelea, jipe moyo kwamba huenda utampata mwingine ambaye ni bora kuliko huyo unayeachana naye.

Kwa leo niishie hapo, tukutane wiki
ijayo kwa mada nyingine nzuri. Kama una ushauri au kuna lolote ambalo
ungependa kulijua, tuwasiliane kwa namba za hapo juu.
tiko
tiko
Post a Comment