tiko
tiko
Santi Cazorla akishangilia na wenzake.
Straika wa Arsenal, Olivier Giroud (wa kwanza kulia) akiifungia timu yake bao la pili.
Olivier Giroud akishangilia bao hilo.
Aaron
Ramsey wa Arsenal akiwatoka wachezaji wa Manchester City, Jesus Navas
(kulia) na Fernando (kushoto) wakati wa mtanange huo.
Kipa wa Arsenal, David Ospina akishangilia ushindi wa timu yake pamoja na beki wake Per Mertesacker (kulia).
KLABU ya Manchester City imepokea kipigo
cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wake wa
Etihad jijini Manchester leo.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya
England, mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Santi Cazorla kwa penalti
huku la pili likifungwa na Olivier Giroud kwa kichwa.
Kwa matokeo ya leo, Manchester City
imeendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 huku ikiwa na pointi
5 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea wenye pointi 52. Asenal wapo
nafasi ya tano wakiwa na pointi 39.
tiko
tiko
Post a Comment