tiko
tiko
Ni matumaini yangu kwamba una shauku
kubwa ya kujua nini nimekuandalia kwa leo. Ni yaleyale kuhusu maisha
yetu ya kimapenzi na leo nataka kuzungumzia usaliti katika sura ya
tofauti.Nimefikia uamuzi wa kuandika juu ya hili kutokana na ushuhuda
nilioupata kutoka kwa mmoja wa wasomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina
la Ashura mkazi wa Arusha.
Ni ushuhuda wa kusikitisha sana lakini una funzo ndani yake kwa wanandoa na wapenzi wa kawaida.
Anasemaje? Hebu msikie kwanza kisha tuendelee; “Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana na hajawahi kunisaliti. Tulioana miaka mitatu iliyopita na sasa nina ujauzito wa miezi nane.
“Mume wangu anafanya kazi na mimi pia nafanya kazi lakini kipato changu ni kikubwa kumzidi mume wangu.
Anasemaje? Hebu msikie kwanza kisha tuendelee; “Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana na hajawahi kunisaliti. Tulioana miaka mitatu iliyopita na sasa nina ujauzito wa miezi nane.
“Mume wangu anafanya kazi na mimi pia nafanya kazi lakini kipato changu ni kikubwa kumzidi mume wangu.
“Kutokana na hali hiyo, mimi nilinunua
gari ambalo mume wangu amekuwa akilitumia muda mwingi. Huwa ananipeleka
kazini kisha yeye anaenda kwenye mihangaiko yake, jioni ananifuata.
“Tunaishi na mdogo wangu wa kike ambaye anasoma chuo ila alionesha
ukaribu sana kwa mume wangu, utani ulikuwa mwingi hadi kuna kipindi
nikahisi kuna kitu nyuma ya pazia.
“Siku moja baada ya mume wangu
kunipeleka kazini, tulimuacha nyumbani yule mdogo wangu, ilikuwa aende
chuo lakini nikashangaa siku hiyo akasema hataenda. “Machale
yakanicheza! Baada ya mume wangu kunifikisha kazini na kuondoka, nikakaa
kama nusu saa hivi kisha nikachukua Bajaj na kurudi nyumbani.
“Huwezi kuamini nilimkuta mdogo wangu
akifanya mapenzi na mume wangu juu ya kitanda changu. Nilipata presha na
kuanguka, nilipozinduka nilijikuta nikiwa hospitalini.“Mpaka sasa niko
kwa wazazi wangu na nakaribia kujifungua. Hivi kwa usaliti huu naweza
kumsamehe mume wangu na tukaishi kwa amani?”
Huo ni ushuhuda wa Ashura ambaye mwisho wa siku aliomba nimshauri. Ingekuwa wewe ungemshaurije? Je, ungemshauri arudi kwa mumewe au ungemtaka aombe talaka?
Huo ni ushuhuda wa Ashura ambaye mwisho wa siku aliomba nimshauri. Ingekuwa wewe ungemshaurije? Je, ungemshauri arudi kwa mumewe au ungemtaka aombe talaka?
Najua kwa vyovyote ungekuwa na la
kumshauri lakini mimi ninavyoona kwa hili ni lazima uwe njia panda.
Yaani mdogo wako umkute kamvulia nguo mumeo na wanafanya uzinzi juu ya
kitanda chako! Ukisikia watu wanaua ni katika mazingira haya.
Hata
hivyo, kabla sijamshauri Ashura nikuulize wewe msomaji wangu, je, upo
usaliti ambao unaweza kusema huu unavumilika na huu hauvumiliki?
Kimsingi watu tunatofautiana jinsi tunavyopokea yale yanayotupata.
Wapo ambao wamewafumania wanandoa wenzao
mara kibao lakini mpaka leo bado wanaishi pamoja na wanasimamia ule
msemo usemao; ‘Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo’.Lakini wakati hao
wakiwa na mioyo hiyo, kuna ambao wameachana baada ya mmoja kukuta tu sms
tata kwenye simu ya mwenza wake.
Kwa hili la Ashura iko hivi, hakuna
usaliti usiouma, uwe ni mdogo au mkubwa. Usaliti aliofanyiwa Ashura ni
mkubwa sana, huwezi kumshauri kirahisi tu kwamba amsamehe mume wake na
arudi kwake.Lakini pia huwezi kumshauri kwamba kwa kuwa ni usaliti
mkubwa basi asimsamehe na aombe talaka.
Ushauri wote unaweza kuwa sawa lakini
pia unaweza usiwe sawa. Kutokana na mazingira, kwamba Ashura ni mjamzito
na mume wake hajawahi kumsaliti, kuna kila sababu ya kusamehe.Kama mume
ameomba msamaha na kuahidi kubadilika, kumgomea itakuwa ni vigumu.
Lakini naomba niseme kwamba, kwenye
suala la usaliti ni vyema tukazungumza na mioyo yetu. Ukijaribu
kufuatilia utabaini hakuna ambaye hajawahi kusalitiwa na mpenzi wake.
Tunachokifanya huwa ni kusamehe na kusahau hasa tukichukulia kwamba,
wote tuna mapungufu. Ni kweli kuna usaliti usiovumilika, kwa mfano kama
amekuwa akikusaliti kila wakati, huyo ifike wakati useme imetosha.
Lakini kama unampenda na kwa bahati
mbaya akawa amekusaliti kwa mara ya kwanza, ni vyema ukampa nafasi
nyingine bila kujali watu watasemaje. Kwa maana hiyo licha ya kwamba
usaliti si mzuri lakini usichukue uamuzi wa kumuacha mwenza wako au
mpenzi wako kwa sababu ya usaliti wa mara ya kwanza, ukifanya hivyo ipo
siku utajuta.
tiko
tiko
Post a Comment