tiko
tiko
Bongomuvi
 kama kawaida walikuwa wamekodisha nyumba ya pedeshe moja washuti muvi 
yao. Kazi ikaanza wakagundua kuwa wanahitaji kuweko na mlinzi, basi 
wakaongea na mlinzi wa kawaida wa nyumba ile na kumwambia kuwa atatokea 
kwenye muvi na watamlipa, mlinzi akakubali.Dairekta akampa panga mlinzi na kumwambia, ‘Nikisema eksheni unaanza kumfukuza yule supasta sawa?” Mlinzi akakubali kuwa kaelewa. Ndipo mambo yakaanza, dairekta akaamrisha, ‘Eksheni’ Basi mlinzi akaanza kumfukuza supasta, akamfukuza mpaka supasta alipofika kwenye ukuta, ndipo dairekta alipotoa amri, ‘Cut cut” Mlinzi akaanza kumkata mapanga supasta, mpaka sasa wako hospitali supasta hali yake ni mbaya sana, tunangoja kujua nani atashtakiwa kwa tatizo hili.
tiko
tiko

Post a Comment