tiko
tiko
Mshtuko! Weka pembeni mahaba niue
waliyokuwa wakioneshana, staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford
amefunguka rasmi kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake ya kimila aliyofunga na
mwanaume wake wa siku nyingi, Dickson ‘Dick’ akikiri kuwa amepoteza muda
mwingi kwa mtu ambaye hakuwa na mapenzi ya dhati kwake.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.
“Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu lakini kuepuka aibu ya kuwa mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema Shamsa.
Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
tiko
tiko
Post a Comment