Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MWANAMKE ASUTWA MCHANA KWEUPE KWA UMBEA..

tiko tiko
 Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina (mwenye nguo nyekundu mbele kushoto), mkazi wa Kawe jijini Dar akisutwa mchana kweupe  na wanawake wanaojiita Cash Money wanakwenda kumsuta.

reproach! The woman mentioned in the name of Sina, a resident 

of 

Kawe Dar has found himself sutwa broad daylight after 

kumvujishia notice his friend called Cheka Komba Mbegere that 

women who call themselves Cash Money going kumsuta, Shooting 

mixture followed step by step.

According to Jamila, who also is a member of Cash Money, Cheka was mgombanisha he and Sheila for kumwaambia be walking with a man named Dumb without knowing one. "This woman has done something very bad, she was going to tell Sheila that I am walking with her husband when we were quarreling frequent and last is that yesterday was ponivamia to beat me when I am drunk.
MSUTO! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina, mkazi wa Kawe jijini Dar amejikuta akisutwa mchana kweupe baada kumvujishia taarifa rafiki yake aitwaye Cheka Komba Mbegere kuwa wanawake wanaojiita Cash Money wanakwenda kumsuta.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo Cash Money walichoshwa na tabia ya umbea wa Cheka ambaye ni memba wa kundi hilo, ndipo walipoamua kumfungia kazi lakini akanusurika baada ya kutonywa na Sina ndipo wamama hao waliobeba ngoma za vidumu vya maji walipomsuta Sina kwa niaba ya Cheka.
Kwa mujibu wa Jamila ambaye naye ni memba wa Cash Money, Cheka alimgombanisha yeye na Sheila kwa kumwaambia kuwa wanatembea na bwana mmoja aitwaye Bubu pasipo kujijua.“Huyu mama amenifanyia kitu mbaya sana, alikuwa anakwenda kumwambia Sheila kuwa mimi natembea na mume wake ambapo tulikuwa tukigombana mara kwa mara na mwisho ndiyo hiyo juzi aliponivamia na kunipiga wakati nimelewa.
Majibizano yakendelea.
“Kwenye ule ugomvi Cheka naye alikuja kunichangia, kesho yake nilipozinduka nilikwenda kituo cha polisi Kawe na kushtaki, asivyo na haya akamuandikia SMS Sheila akimwambia waende kwa mganga ili eti waifute kesi,” alisema Jamila.
Baada ya kuona mambo yameshindakana kwa mganga, Sheila akaona bora amuombe msamaha Jamila ndipo walipomjua ‘mchawi’ wao ni Cheka kisha wakaungana kwenda kumsuta.
“Nilipoona mambo yamenifika shingoni nikaona nirudi kwa mwenzangu nimuombe msamaha tupatane, ndiyo nikamweleza mtu aliyekuwa akituchonganisha tukapanga siku ya kumsuta ambayo ndio leo lakini bahati yake akawa ametonywa akakimbia, tulichunguza tukabaini ametonywa na Sina ndipo naye tukamsuta barabara,” alisema Sheila.
Wakizidi kusutana.
Paparazi wetu aliwashuhudia Cash Money wakimuimbia Sina nyimbo za kumsuta huku wakipiga ngoma za vidumu vya maji kwa takriban nusu saa ambapo Sina alileta vurugu kali ya kutaka kujinasua lakini hakufanikiwa.
“Hii ndiyo kiboko ya wambeya, kwa aliyeona fedheha hii kamwe hawezi kufanya umbeya wa aina yoyote,” alisikika shuhuda  mmoja.
Baada ya kumalizika kwa tukio hilo, paparazi wetu alimvutia waya Cheka ili kumuuliza kama ni kweli alihusika kuwagombanisha Jamila na Sheila na sababu za yeye kutimka nyumbani hapo siku ya tukio.“Mimi nilikimbia kwa sababu walisema eti wamewaita waandishi waje wanisute lakini ukweli ni kwamba mimi sijawahi kuwachonganisha ila walipopigana nilikwenda kuwasuluhisha.
“Hata hivyo wale hawanipendi kwa sababu nimejitoa kwenye kundi lao na ninawadai hela zangu ndio maana wananichafua,” alisema Cheka.   Hata hivyo, Cash Money waliahidi kufanya msuto ‘party two’ muda wowote watakapomtia mikononi Cheka wakidai wamechoshwa na tabia yake ya kuwagombanisha watu.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top