tiko
tiko
Profesa huyo akiwa na wahadhiri pamoja
na watu wengine walioelezwa kuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani
Dodoma walifanya maandamano hayo Machi 22, mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, uongozi wa Udom
umemtaka ajieleze kwa nini ameshiriki harakati hizo za kisiasa huku
akijua kuwa ni mtumishi wa umma anayepaswa kuwahudumia watu wenye
itikadi tofauti.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris
Kikula alisema kwa kuwa jambo hilo lilionekana kukiwakilisha chuo
katika masuala ya siasa, uongozi ulilazimika kumhoji mhadhiri huyo.
“Ametuandikia barua ya kujieleza na
kubainisha kuwa alikwenda yeye binafsi na siyo kama mwakilishi wa chuo.
Lakini mambo haya ni magumu sana kutofautisha. Mimi kwa mfano, siwezi
kwenda sehemu halafu nikasema sikwenda kama mkuu wa chuo kwa sababu
siwezi kutofautisha hilo. Lakini tumechukua maelezo yake na
tumeyahifadhi,” alisema Profesa Kikula.
Kuhusu wanafunzi wanaodaiwa kushiriki
harakati hizo kutoka chuoni hapo, alisema hakuna wanachoweza kufanya kwa
sababu mbili kubwa. Kwanza, ni vigumu kuwatambua waliofanya hivyo na
pili walifanya hivyo nje ya chuo, jambo linalowezekana.
“Maandamano hayo yalifanyika mtaani.
Huko walikuwa wanavunja sheria za nchi, kama hayakufuata sheria, Jeshi
la Polisi ndilo lenye mamlaka ya kudhibiti au kuruhusu jambo kama hilo
kufanyika,” alisema. Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Profesa Kopoka
alikiri kuandika barua hiyo na kueleza kuwa alichokifanya ni kutekeleza
haki yake ya uraia ya ushiriki katika utawala wa haki na demokrasia
nchini.
“Nimefanya hivyo. Nilikwenda kutokana na
imani yangu kutokana na vile ninavyomfahamu Lowassa. Sikuwa peke yangu.
Ni kama ilivyoripotiwa, walikuwapo pia wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya
Mtakatifu Yohana (St. John) na Mipango,” alisema Profesa Kopoka.
Alisema pamoja na kufanya hivyo, suala hilo halijaathiri utendaji wake wala mkataba wake wa ajira.
Mfululizo wa kukanusha
Siku nne baada ya maandamano hayo,
viongozi wa Serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali
walijitokeza na kukanusha habari hiyo kwa maelezo kuwa waliofanya hivyo
hawakuwa wanafunzi na wala suala hilo halikupata baraka kutoka vyuoni.
Katika taarifa ya pamoja ya marais wa
serikali za vyuo vikuu hivyo vilivyomo mkoani humo iliyosomwa na Rais wa
St. John, Daniel Daniel imepinga kushiriki kwao na kubainisha kuwa
waliofanya hivyo ni watu wa mtaani.
tiko
tiko
Post a Comment