tiko
tiko
Mapenzi ya sasa yamejaa sarakasi nyingi sana, kwa yule aliyebahatika
kuingia kwenye uhusiano anatakiwa kuwa makini kuhakikisha mapenzi
hayamtibulii maisha yake.Yapo mambo mengi ya kuwa nayo makini,
changamoto kubwa na ya msingi ambayo wengi tunakumbana nayo ni uhakika
kama kweli wanaodai wanatupenda wanamaanisha au wana zuga?Kwamba
yule anayesema anakupenda ukimpasua kwenye moyo wake wewe utakuwa ndiye
uliyechukua nafasi? Wengi wamebaki njia panda wanapofikiria hilo.Mbali
na changamoto hiyo, pia wengi hufikiria namna ya kulinda penzi lisife.
Wapo waliotokea kupendana sana lakini wakaishia njiani kwa kuachana.
Lakini pia wapo ambao mpaka leo hii wanajiuliza kama waliotokea
kuwapenda wana nia njema? Kwamba anayekuambia anakupenda na anatamani
siku moja uwe mwenza wake anamaanisha kweli au ana lake kichwani?
Kama ulikuwa hujui ni kwamba, wapo wanaume ambao wamejiwekea malengo ya
kutembea na idadi flani ya wanawake kwa kipindi flani. Kwa hiyo wewe
unayo changamoto ya kubaini kama huyo uliye naye siyo kati yao!
Achilia mbali hao wanaume, wapo wanawake pia ambao kazi yao ni kubadili wanaume kila siku, akifuatwa na mwanaume hawezi kusema ‘no’, atamkubalia.
Achilia mbali hao wanaume, wapo wanawake pia ambao kazi yao ni kubadili wanaume kila siku, akifuatwa na mwanaume hawezi kusema ‘no’, atamkubalia.
Atakuwa naye kwa kipindi flani huku kuchuna ikiwa ni sehemu ya maisha
yake kisha baada ya muda anamuacha. Ndiyo maana nikaanza kwa kusema
kuwa, maisha ya kimapenzi ya sasa yamejaa changamoto nyingi sana.
Hata hivyo, kubwa ambalo leo nataka kulizungumzia linahusu hii tabia ya
baadhi ya wapenzi wanapokuwa faragha kupigana picha za utupu! Hakika
hili linanishangaza sana na nahisi wanaofanya hivyo hawana akili timamu.
Huwa najiuliza, mwanaume au mwanamke anapochukua simu au kamera kisha
kumpiga au kumrekodi mpenzi wake akiwa kama alivyozaliwa ni ili iweje?
Anazipiga kwa ajili ya matumizi gani? Ni swali ambalo hata wewe mwenye
akili timamu unaweza kuwa unajiuliza.
Katika kujua kilicho nyuma ya pazia, nilijaribu kuzungumza na baadhi ya
wanaume ambao ndiyo wanaotajwa sana kufanya kamchezo hako. Wapo
waliosema wanafanya hivyo kwa kujifurahisha tu lakini wengine wakasema
eti ni ili wanapokuwa mbali na wapenzi wao wapate kitu cha kujiliwazia.
Si
wanaume tu wanaosema hivyo, hata baadhi ya wanawake nao walisema
hivyohivyo. Lakini sasa cha ajabu wapo waliokuwa wawazi zaidi kwa kusema
kuwa, wanawapiga picha wapenzi wao wakiwa watupu ili wakigombana
wazitumie kuwakomoa. Yaani mwanaume anampiga picha mpenzi wake ili siku
wakikorofishana au akitaka kuachwa, aziachie kwenye mitandao ili
kumkomoa.
Sasa, ukiacha zile sababu nyingine, tusimamie hii ya kwamba wengi
wanazipiga ili wakigombana na wapenzi wao wawaaibishe. Wewe ambaye una
akili zako timamu unakubalije kupozi mbele ya kamera na kumruhusu
mpenzi wako akufotoe?
Hebu tuache huu ulimbukeni. Kupigana picha tukiwa watupu ni kinyume na
maadili na sheria za nchi. Ukiona mpenzi wako anachukua simu yake kisha
kutaka kukupiga picha, chukulia huyo hakupendi na siku hiyo iwe ndiyo
mwisho wa uhusiano wenu.
Ninachokushauri msomaji wangu uliye kwenye uhusiano ni kwamba, ukiwa
faragha na mpenzi wako hata kama unampenda na unamuamini sana, kuwa
makini naye. Sasa hivi kwa teknolojia ilivyo watu wanapiga picha kwa
siri kiasi kwamba ukizubaa utashangaa siku unaambiwa picha zako za utupu
zipo, unabisha kumbe umepigwa na mpenzi wako bila wewe kujua.
Huwezi kuamini wapo watu wako kwenye ndoa lakini ukipekua simu zao wana
picha za wake zao au waume zao wakiwa watupu, sasa kwa wapenzi wa
kawaida hali ikoje?
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment