tiko
tiko
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
Harakati
za Uchaguzi Mkuu zimeendelea kushika kasi, baada ya utafiti uliotolewa
jana kumtaja Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kuongoza kundi la
wanasiasa vijana wanaokubalika na Watanzania katika kugombea nafasi ya
urais.
Akizungumza
jijini Dar es salaam jana wakati akizindua ripoti ya utafiti uliofanywa
na Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Elimu (Tedro), Mwenyekiti wa
taasisi hiyo, Jacob Kiteli, alisema Nchemba aliongoza kati ya wanasiasa
vijana saba waliotajwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na upinzani.
Alisema
utafiti huo ulifanyika katika wilaya 18 na vijiji 54, ulikuwa na lengo
la kutathimini ushiriki wa vijana katika siasa katika kugombea na
kutekeleza wajibu wao kwenye madaraka kwa maendeleo ya jamii.
Alisema
katika kipengele cha mtu gani anaweza kupita katika uchaguzi endapo CCM
itampendekeza, Nchemba alipata asilimia 38 na kufuatiwa na January
Makamba aliyepata alama ya asilimia 24.
Wengine
waliotajwa na alama zao kwenye mabano ni William Ngeleja (11), Lazaro
Nyalandu (10), Dk. Hamisi Kigwangallah (7), Deo Felikunjombe (5) na
Esther Bulaya (2).
Utafiti
huo pia umebaini kuwa mgombea kijana ambaye angeshinda kwenye
kinyang’anyiro hicho bila kujali itikadi za vyama, Nchemba ameongoza kwa
asilimia 27, akifuatiwa na Zitto Kabwe (Chadema) kwa asilimia 19.
Wengine na asilimia zao kwenye mabano ni Makamba (14), James Mbatia (10), Tundu Lissu (14), Nchimbi (8) na Nyalandu (7).
Kwa upande wa upinzani, vijana wanaoonekana kuwa na ushawishi mkubwa ni Zitto (19), Mbatia (11), Lissu (5) na Halima Mdee (4).
Akizungumzia
kuhusu chama chenye nafasi kubwa ya kushinda iwapo uchaguzi ungefanyika
leo, Kiteli alisema utafiti umebaini kuwa CCM bado ina nafasi kubwa
ikiongoza kwa asilimia 53.4.
Katika
kundi hilo, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinafuatia kwa
asilimia 27. 3, kikifuatiwa na Cuf (7.3) na NCCR-Mageuzi (4.4).
Kiteli alisema Watanzania wengi wana amini vijana wana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya haraka ya kiuchumi na kisiasa.
“Asilimia 82 ya waliohojiwa walikubali kumpigia kura mgombea urais kijana, 11 walikataa na saba walisema hawajui,” alisema.
Alisema
utafiti huo unaonyesha katika chaguzi vijana wengi waliojitokeza
kugombea nafasi mbalimbali, baadhi yao walishinda na wengine kushindwa.
“Sababu
ya vijana kushindwa katika uchaguzi inatokana na kukosa fedha za
kuendesha kampeni, kutojipanga vyema kukabiliana na wapinzani wao pamoja
na kupewa rushwa ili wajitoe,” alisema Kiteli.
Hata
hivyo, Kiteli alifafanua kwamba utafiti huo haukuegemea vyama vya
kisiasa wala makundi ya kijamii, badala yake iliegemea kujua mahitaji ya
wananchi juu ya viongozi wanaowahitaji.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment