tiko
tiko
Klabu ya Manchester United
imeendelea kutowaridhisha mashabiki wake baada ya mfululizo wa matokeo
ambayo si mazuri ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata, mpaka sasa inashika
nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Moja kati ya rekodi ambazo mashabiki wa United
hawatazipenda ni ile inayoonyesha kuwa timu hii haijaweza kushinda
mchezo hata mmoja ambao imeanza kuruhusu bao kufungwa na mpinzani wake.
Katika msimu huu United
wameruhusu bao la kwanza la mchezo kufungwa na mpinzani katika michezo
nane tofauti na hadi sasa hakuna mchezo wowote kati ya hiyo ambao United imeweza kurudi na kushindwa zaidi ya kuambulia sare kama si kupoteza.
Katika ya mechi hizo United imeweza kusawazisha mara tano ambapo michezo hiyo iliisha kwa huku ikipoteza mchezo katika michezo mitatu iliyosalia.
Michezo ambayo imeisha kwa sare baada ya United kufungwa bao la kwanza ni dhidi ya Chelsea, West Brom, Aston Villa, Stoke City na West Ham United huku wakipoteza michezo dhidi ya Manchester City, Swansea na Southampton.
Katika miaka ya nyuma United
ilijijengea umaarufu kama timu ambayo ilikuwa haikubali kirahisi
kuondoka uwanjani bila kushinda mchezo na mara nyingi walishinda mechi
ambazo awali ilionekana kama wangepoteza kabla ya kurudi mchezoni na
kushinda mchezo karibu na mwisho wake.
Hii ilizoeleka kipindi wakati Sir Alex Ferguson akiwa kocha na hata alipokuja David Moyes bado United ilifanikiwa kushinda michezo minne ambayo ilianza kufungwa mapema.
Katika msimu wa mwisho wa Sir Alex Fergusson, United
walionekana kuwa wataalamu wa kushinda mechi ambazo zingeweza kuwa za
kupoteza baada ya kurudi mchezoni kwa kusawazisha na kufunga bao au
mabao ya ushindi katika mechi zisizopoungua tisa ikiwa idadi kubwa ya
matokeo ya aina hiyo katika miaka yote 26 ambayo United ilikuwa chini ya ‘babu’.
Nitaendelea kukupatia kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment