tiko
tiko
Valentines Day ama kwa Kiswahili Siku ya Wapendanao, huadhimishwa kila
Februari 14 ambapo kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, siku hiyo
inazidi kuwa maarufu na kuadhimishwa kwa shangwe ingawa wengi hushindwa
kuelewa hasa maana yake.
Ukiwauliza
wengi nini hasa maana ya Valentines Day, ni wachache wanaoweza
kukueleza kwa ufasaha maana yake na kwa sababu hiyo, wengi wanakuwa na
kawaida ya kuiadhimisha siku hiyo kwa mazoea tu, huku wakifanya mambo
ambayo hayafai mbele ya jamii.
HISTORIA YA SIKU YA WAPENDANAO
Mtakatifu Valentine ndiye hasa muasisi wa Siku ya Wapendao ambapo karne nyingi zilizopita, katika utawala wa Warumi, alikuwa akipita kwenye magereza ya wafungwa wa kivita na kambi za wanajeshi, akiwahubiria watu habari za kuwa na upendo kati yao.

Mtakatifu Valentine hakuishia hapo, alifanya pia kazi ya kuwafungisha
ndoa kwa siri wanajeshi wa Kirumi ambao hawakuwa wakiruhusiwa kuoana
wawapo kambini. Kazi hiyo ya kuwafungisha ndoa na kuhubiri upendo,
ilisababisha Mtakatifu Valentine akamatwe na kutupwa gerezani kwa
kuvunja sheria za utawala wa Kirumi.
Akiwa gerezani, Mtakatifu Valentine aliendelea na kazi yake ya
kuwahubiria wafungwa wenzake upendo, kuwasaidia waliokuwa wagonjwa kwa
kuwaponya, kuwafungisha ndoa wanajeshi kwa siri na kuendeleza huduma za
kiroho zikiwemo kuwaombea watu wenye matatizo mbalimbali.
Kesi yake iliendelea kuunguruma, akishtakiwa kwa kosa la kuwafungisha
ndoa wanajeshi wa Kirumi, jambo ambalo lilikuwa ni kinyume na sheria za
kipindi hicho, mwisho akahukumiwa adhabu ya kifo.Akiwa anaendelea
kusubiri siku yake ya kunyongwa, mtoto wa mkuu wa gereza alilokuwa
amefungwa aitwaye Asterius, alipatwa na maradhi ya ajabu ambayo
yalisababisha akaribie kukata roho.
Mtakatifu huyo aliposikia habari hizo, aliomba kwenda kuonana naye
ambapo alimponya maradhi yaliyokuwa yanamsumbua. Habari za tukio hilo la
kipekee, lililodhihirisha upendo wa dhati, zilisambaa kwa kasi ndani na
nje ya gereza.
Siku
chache kabla Mtakatifu Valentine hajanyongwa, alimuandikia barua ya
kumuaga binti huyo wa mkuu wa gereza, chini kabisa akaandika maneno
‘Your Valentine’, akaambatanisha na ua waridi jekundu.
Hata aliponyongwa na kufa, wafuasi wake waliokuwa wakiyakubali mafundisho yake, waliendelea kuiadhimisha siku aliyonyongwa, Februari 14 kwa kupeana kadi na barua zenye maneno ‘Your Valentine’ au ‘To My Valentine’ kudhihirisha upendo waliokuwa nao kwa wahusika.

TAFSIRI SAHIHI
Kwa kuitazama historia hiyo fupi, tunajifunza kuwa kumbe Valentines Day siyo siku ya kufanya ngono hovyo, kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, kulewa na kufanya kufuru nyingine kama hizo bali ni siku ya kuoneshana upendo, kupeana zawadi zikiwemo kadi nzuri, maua na chocolate.

Na unayemfanyia hivyo, siyo lazima awe mpenzi wako, anaweza kuwa mama
yako, baba yako, rafiki yako, mwanao au mtu yeyote unayetaka
kudhihirisha kwamba unampenda, ingawa pia wanandoa (waliohalalishwa)
huitumia siku hii kuongeza mapenzi kwenye ndoa zao kwa kupeana zawadi na
kutoana ‘out’, wakiwa katika mavazi maalum ya rangi nyekundu.
Ni matumaini yangu kwamba msomaji wangu utakuwa umepata mwanga kuhusu
maana na tafsiri ya Valentines Day. Nakushauri na wewe usiwe miongoni
mwa watu wanaofuata mkumbo kwa kuiadhimisha siku hii tofauti kabisa na
maana yake halisi. Epuka kufanya ngono hovyo au kukesha gesti kwa
kisingizio cha kuadhimisha Valentines Day kwani hiyo siyo tafsiri yake.
Tukutane tena wiki ijayo, Happy Valentines Day.
Tukutane tena wiki ijayo, Happy Valentines Day.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment