tiko
tiko
Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ameeleza
kushangazwa kwake na taarifa zinazozidi kuenea kuwa amejifungua, jambo
ambalo anadai eti siyo kweli.
Madai ya staa huyo kujifungua kwa siri yameenea na hata wasanii wenzake
wanajua hivyo lakini mwenyewe amekuwa akikanusha na kuwaacha mashabiki
wake njia panda.Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Snura alisema
yeye ana mtoto mmoja mkubwa lakini madai ya kwamba amejifungua hivi
karibu hayana ukweli.
“Mimi sina mtoto mdogo, mwanangu ni yule mnayemjua, hao wanaosema
nimezaa mbona wananizalisha?” alihoji Snura ambaye baada ya muda mrefu
kupotea, juzikati aliibukia kwenye Ukumbi wa Escape One ulipo Msasani,
jijini Dar.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment