tiko
tiko
Alitoa kauli
hiyo jana jioni wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere,
baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu
kwenye Shule ya Sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.
Waziri Mkuu
alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji
yaliyokwishawasilishwa na watakapopata mgawo wao, hawana budi
kuangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa
shule hiyo.
Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara, Waziri Mkuu alisema:“Mkoa mzima wa Iringa unahitaji maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108.
“Lakini kuna
nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua nzuri.
Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249
zilizokamilika,” alisema.
“RC inabidi
uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo hazijaanza kujengwa zikamilike
kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyoelekeza.
Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi,” aliongeza.
Alisema elimu ni
sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu wa kipekee na
kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini ya Mpango
wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).
Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu, ili wafanye vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Mapema, akitoa
taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Ofisa Elimu wa Wilaya ya Iringa, Leonard
Msigwa, alisema ujenzi wa nyumba hizo nne zenye pande mbili, umegharimu
Sh milioni 323.2.
Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko, zina uwezo wa kubeba familia nane.
Msigwa alisema
ujenzi wa nyumba hizo ulifanywa na shirika la Deswos la Ujerumani kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na wananchi.
Pia walisaidiwa
kujengewa tangi la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana.
Akifafanua
kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Ofisa Elimu huyo alisema hadi sasa
wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Bayoolojia, lakini
bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Aidha mfumo wa gesi na maji
umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.
“Ujenzi wa
maabara hadi sasa umekwisha gharimu Sh milioni 52.8/- na kwa Februari
2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya samani za maabara yaani meza 24
na stuli 96 zenye thamani ya Sh milioni 8.9,” alisema.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment