tiko
tiko
HALI bado
ni tete kwa mwenyekiti wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) lakini wakakosa ajira, George Mgoba kufuatia kutekwa kwake
na kujeruhiwa vibaya hivi karibuni na watu ambao bado hawajajulikana.
Mwenyekiti
wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini
wakakosa ajira, George Mgoba akiwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili .
Mgoba ambaye mpaka juzi alikuwa bado amelazwa katika Hospitali ya Mkoa
wa Ilala, Amana jiijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa, simulizi yake
inaonesha kichwani kumejaa msongo mkubwa wa mawazo kutokana na watu
waliomteka kumlazimisha kufanya mapenzi na mwanamke mmoja.
Kwa mujibu wa Mgoba, mwanamke huyo alikuwa mweupe, ana umri wa kati na
wakati wanamlazimisha kufanya naye mapenzi yeye hakuonesha kukerwa,
inaonekana alikuwa anajua.
“Kilichonishinda kufanya naye mapenzi yule mwanamke ni mwili kuishiwa
nguvu na pia sehemu zangu za siri zilikuwa zina maumivu makali sana.
sijajua nia yao ilikuwa nini kama ningefanikiwa,” alisema Mgoba.
Habari kutoka chanzo kimoja ndani ya jeshi la polisi, mwanamke huyo alitakiwaa kutumika maalum ili Mgoba aseme kila kitu kwa maswali ambayo angeulizwa na waliomteka.
Habari kutoka chanzo kimoja ndani ya jeshi la polisi, mwanamke huyo alitakiwaa kutumika maalum ili Mgoba aseme kila kitu kwa maswali ambayo angeulizwa na waliomteka.
“Ile ni njia ya kupata ukweli, huwa inatumika. Mtu anaweza kupewa
mwanamke afanye naye mapenzi kwa lengo la kumchunguza. Si unajua wanaume
wanapobanwa kwenye kona ya mahaba wanajiachia hata kwa mambo ya siri
wao wanasema tu,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “We unadhani Samson (kwenye Biblia), kama si yule mwanamke
wake Delila angesema siri ya nguzu zake?”Baadhi ya watu wameunganisha
kitendo cha kutekwa kwa Mgoba kilichotokea Ijumaa iliyopita, Mabibo Dar
na kwenda kutupwa mkoani Pwani ni harakati zake za kuwaongoza wenzake
kuandamana kwenda Ikulu, Dar kwa lengo la kuonana na Rais Kikwete kudai
wapewe ajira.
Juzi saa mbili na nusu asubuhi, Uwazi lilifika Hospitali ya Amana baada
ya kuwepo kwa taarifa kwamba, Mgoba ataongea na waandishi wa habari.
Hata hivyo, mpaka Uwazi linaondoka saa tisa, Mgoba hakufanya hivyo huku
polisi wanaomlinda na wauguzi wanaomtibu wakidai hawana mamlaka ya
kumruhusu majeruhi huyo kuzungumza na vyombo vya habari.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment