tiko
tiko
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoani Iringa imewafikisha
mahakamani mkuu wa wilaya ya Mufindi mkoani humo Bibi Evarista Kalalu,
mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara mikindani Limbakisye Shimwela pamoja
na mkurugenzi wa halmashauri ya Biharamulo mkoani Kagera Bwana Nasib
Mbaga wakishitakiwa kwa makosa sita ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka.
Washtakiwa
waliofikishwa mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo
Victoria Nongwa ni pamoja na mkuu wa wilaya Kalalu, alitekuwa
mkurugenzi wa halmashauri ya mufindi Limbakisye Shimwela ambaye kwa sasa
yupo Mtwara Mikindani, aliyekuwa afisa mipango Nassib Mbaga ambaye sasa
ni mkurugenzi mtendaji wa Biharamulo, mhandisi Cosmas Mduda, na
mkandarasi Fredrick Msimbwa.
Mwendesha
mashataka wa Takukuru Imani Nitume amedai mbele ya hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama hiyo ya wilaya ya Mufindi Victoria Nongwa kuwa
washatakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Decemba 2010 na February
2011 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa ambapo walikula njama ya kula
rushwa kinyume na sheria ya Takukuru na sheria ya manunuzi ya umma na
kuingi mkataba wa ujenzi wa vyoo, mabafu na mfumo wa maji na
kusababishai halmashauri hiyo hasara ya shilingi milioni tatu.
Washatakiwa
hao wote wamekana mashitaka hayo na wapo nje kwa dhamana ya shilingi
milini moja kila mmoja wakidhaminiwa na wadhamini wawili kila mmoja
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment